WATU 20 WAFA KWA KIU


**************************************



Maafisa wa uokozi wa Libya wamepata miili ya watu 20 jangwani karibu na mpaka na Chad.

 Watu hao waliokufa wanaaminika kuwa wahamiaji na walipatikana karibu na gari jeusi aina ya 'pickup'. 

Gari hilo liligundulika karibu kilomita 320 kusini magharibi ya mji wa Libya wa Kufra. 

Waokozi wamesema watu wote 20 walikufa kutokana na kiu baada ya gari lao kuharibikia jangwani. 

Katika tukio jingine tofauti lililotokea katika pwani ya Libya, boti ya mpira ilizama ikiwa imewabeba watu 30.

 Meli ya uokozi ilifanikiwa kuifikia boti hiyo na kuwaokoa watu kadhaa - ijapokuwa wanawake watano na watoto wanane hawajaonekana na inadhaniwa wamekufa.


#Dwkiswahili

0/Post a Comment/Comments