************************************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kufanya huduma zake za Airtel Money kuwa nafuu pamoja na kuhimiza matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi kwa watumiaji wa Airtel Money na wale ambao si watumiaji kwa kuzindua promosheni ya Airtel Money Bila Tozo.
Hatua hii imekuja baada ya kufanyika kwa urekebishaji wa tozo kwenye miamala ya simu za mkononi pamoja na serikali.
Kwenye taarifa yake, Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda alielezea jinsi Airtel imeendeleza dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za serikali kwa kurahishisha gharama za kufanya miamala ya simu za mkononi.
Alisema kuwa Airtel itaondoa gharama ya tozo kwenye kutuma au kupokea fedha kwa kiwango cha 001-29,000 Airtel kwenda Airtel.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza promosheni hii, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema ‘Hatua hii ya Airtel kuondoa tozo ni juhudi za Airtel kuhimiza huduma za kifedha pamoja na suluhisho la kifedha nah ii ni baada ya kuona jinsi huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi zilivyobadilisha uchumi ya kifedha kwa wananchi.
Nchunda aliongeza kuwa wateja wengi wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi hawana akaunti za benki, na kiwango chao cha kutuma au kutoa fedha huwa mara nyingi ni mpaka 29,999.
Kwa punguzo la tuzo kwenye kutuma na kutoa kutawafanya wateja wa Airtel kutuma na kutoa fedha bila ya maumivu ya tozo.
Kwa hivi kutawafanya wateja wa Airtel na hasa wenye uchumi wa chini kufanya miamala yao kwa unafuu na kwa Uhuru zaidi.
Vile vile, kwa mteja wa Airtel anayetumia Applikesheni ya Airtel kwa kutuma fedha Airtel kwenda Airtel, atatuma bila tozo kwa kiwango chochote kile.
Nchunda aliongeza kuwa Airtel wanayo Imani kuwa promosheni hii ya Bila Tozo itawafanya Watanzania kuendelea kufanya miamala kwa Uhuru na kuchangua Airtel Money kuwa changua lao kwenye



Post a Comment