Katibu mkuu wa machinga mkoa wa Dar es salaam ndugu Masudi Chauka akiongea na wandishi wa habari.
baadhi ya majiko yaliyopo kwenye mitaa ya kariako na hapa ni Wakati wa portion ya kuwaondoa iliyoendeshwa leo na Katibu mkuu wa machinga mkoa wa Dar es salaam ndugu Masudi Chauka
...................
Na Mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Masudi Chauka amesema chama Cha wafanya biashara ndogo ndogo (machinga) mkoa wa Dar es salaam kimeanzisha operation ya kuwahamisha wafanya biashara wenye majiko katikati ya mitaa ya Kariako Ili kuondoa adha wakati wa ufanyaji wa Biashara.
Amesema majiko katikati ya mitaa hayakubaliki kwa sababu yanaweza kuleta athari kubwa ikiwa moto huo ukiwaka ndani ya mitaa hiyo na kuweza kuteketeza majengo ambayo mengi yao yana stoo za mizigo ya wafanya biashara.
Aidha ameongeza kuwa kumekuwepo na ongezeko la wafanya biashara wapya ndani ya mitaa ya Kariakoo na wanakuja na biashara ya majiko ambayo ni hatari kwa maeneo hayo
Aidha amesema kuwa kumekuwapo na baadhi ya maneno ya upotoshaji yanaendelea mitandaoni kwamba wanakamata mizigo ya wafanyabiashara na Kisha kuwaomba rushwa ndo wawarudishie mizigo yao habari ambazo amezikanusha kuwa sio kweli.
"tunafanya operesheni hii ya kuwaondoa wamachinga ambao wamekuja kwenye mitaa ambayo tuliomba serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa kwa ajili ya kufanya biashara zetu ambayo tulijipanga vizuri kwa kupanga meza na kuacha njia za watembea kwa miguu"
Pia amesema wameweka utaratibu mzuri ambao uliwezesha watu kupita vizuri pindi wawapo Kariakoo kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na wakiacha njia za gari Ili yaweze kupita kwa urahisi hata wenye maduka wasipate taabu yakupitisha au kushusha mizigo yao.
"Naomba serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ituongezee mitaa ya kufanyia biashara kwasababu mahitaji ni mengi, huku tukisubiri kujengewa soko letu pale Eneo la jangwani"
Ameongeza kuwa wanaendelea na operation ya kuwahamisha wale wote walitoka kwenye barabara ya Mwendokasi ambao hawafuati utaratibu bali wanavamia maeneo na kupanga biadha zao chini hali ambayo inapelekea kuleta kero katikati ya mitaa hiyo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa njia hizo.



Post a Comment