*********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mh. Anthony Mavunde amewahakikishia wananchi wa mtaa wa Muungani kata ya Mbalawala kumalizia ujenzi wa shule mpya ya Msingi katika eneo la Muungano ili kupunguza mwendo wa watoto wa shule wanaotembea umbali mrefu kuifuata Shule ilipo hivi sasa
Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Mbalawala ambapo moja ya hoja iliyojitokeza ni hiyo ya umbali mrefu wa wanafunzi wanaotembea kufuata shule.
Shule hiyo inajengwa na Mbunge Mavunde kwa ushirikiano na wananchi wa Mtaa wa Muungano ambapo Mbunge huyo amechangia Tsh 5,000,000 na mifuko 50 kuunga mkono jitihada za wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Mbalawala Mh. Charles Ngh’ambi, amemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada za kusimamia utekelezwaji wa mradi wa umeme katika kata hiyo pamoja na utatuzi wa changamoto mbalimbali za ndani ya kata hiyo.
Mwisho.



Post a Comment