Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametembelea mabanda mbalimbali katika uwanja wa Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Katika ziara yake Dk Mwinyi ametembelea banda la Benki ya Azania, Tan Trade na Mabanda mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yakiwemo ya Helwan factory wanaojihusisha na utengenezaji wa Enjini za Treni, banda la China na India, Banda la Zanzibar, Benki ya Watu wa Zanzibar-PBZ, Property International: waliojikita na uuzaji wa viwanja, banda la Wafanyabiashara Wanawake na banda la mwisho lilikuwa la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Katika ziara yake Rais Dk. Mwinyi alieleza kufurahishwa na Bidhaa na Teknolojia zinazovutia kwenye mabanda aliyotembelea.
Pia alifahamisha utayari wa Serikali zote mbili kuzisaidia Kampuni na Viwanda hivyo katika Soko la Dunia. Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi alirejea Zanzibar mara baada ya ya ziara hayo.



Post a Comment