Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw.Christopher Mramba akipata picha ya pamoja na washindi wa mwaka 2021/2022 wa tuzo za kitaifa za Ubora kwenye hafla ya Utoaji wa Tuzo hizo leo Julai 14,2022 iliyofanyika Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
**************************
Na James Salvatory (Torch Media)
Tasisi za sekta binafsi nchini zimetakiwa zisaidie kuhamasisha wanachama wake kushiriki kwenye mashindano ya tuzo za kitaifa za Ubora kwa washindi ili kufanikisha kupata washindani bora katika ngazi ya jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).
Ameyasema hayo leo Julai 14,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Christopher Mramba kwenye hafla ya Utoaji wa Tuzo za kitaifa za Ubora kwa washindi wa mwaka 2021/2022.
Amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iliona umuhimu wa kuanzisha Tuzo za ubora za Kitaifa na kutoa jukumu la kuziratibu kwa Shirika la Viwango Tanzania pamoja na TPSF.
Aidha amesema washindi wa tuzo hizo watapata fursa ya kushiriki kwenye mashindano ya tuzo za ubora kwa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya maendeleo kwa Nchi kusini mwa Afrika (SADC) na hivyo kupata nafasi ya kufahamika na kupata masoko zaidi.
Hata hiyo ameitaka TBS Kuwekeza kwenye kutangaza mashindano hayo yajulikane na wahusika ili kuhamasisha washiriki wawe wengi zaidi kwa mwaka ujao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa David Ndibalema amesema Katika zama hizi tulizopo ni ngumu kuzuia bidhaa na huduma kutoka kwenye nchi moja kuuzwa kwenye nchi nyingine kutokana na uwepo wa kanuni za kimataifa hususani kanuni za WTO.
Katika hatua nyingine sekta binafsi zimetakiwa kuzingatia utamaduni wa ubora na viwango katika kila kitu kinachozalishwa ili kuweza kuwa na vitunavyotakiwa katika soko kwa ujumla.
MWISHO




Post a Comment