Watu nane wameuawa na vikosi vya usalama nchini Sudan wakati maelfu ya waandamanaji wanaodai demokrasia walipoingia barabarani jana wakiendelea kupinga utawala wa kijeshi na kutaka uongozi wa kiraia.
Tume ya madaktari wa Sudan imesema katika taarifa yake kwamba raia sita waliuawa kwa kupigwa risasi wakati polisi walipofyatua risasi za moto dhidi ya waandamanaji katika mji pacha wa Omdurman.
Mwandamanaji mwingine alifariki mjini Khartom kutokana na jeraha la risasi ya kichwa wakati mtoto mmoja naye akipoteza maisha baada ya kupigwa risasi ya kifua.
Mjini Khartoum, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji.
Maandamano ya jana pia yameangukia katika kumbukumbu ya miaka mitatu ya maandamano ya umma ya mwaka 2019 yaliyomwondoa mamlakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir
#DwKiswahili

Post a Comment