Ibada kubwa kabisa ya hajj tangu kuzuka kwa janga la Corona imeanza jana, huku mamia kwa maelfu ya waumini, wengi wao wakiwa bila ya barakoa wakianza kumiminika katika eneo takatifu kabisa la dini ya Kiislamu, Mecca nchini Saudi Arabia.
Waislamu milioni moja waliochanjwa, wakiwemo 850,000 kutoka mataifa ya kigeni, wanaruhusiwa katika hajj ya mwaka huu, ikiwa ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka miwili iliyopita wakati idadi hiyo ilipunguzwa kutokana na janga la corona.
Katika mwaka wa 2019, waumini milioni 2.5 wa Kiislamu kutoka kote ulimwenguni walishiriki katika ibada hiyo ya Hajj inayoandaliwa kila mwaka, na ambayo ni nguzo ya mwisho katika nguzo tano za imani ya kiislamu.
Waislamu wenye uwezo wa afya na kiuchumi wanatakiwa alau mara moja katika uhai wao kuitimiza nguzo hiyo.
#Dwkiswahili

Post a Comment