Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kujiuzulu na kumaliza mgogoro wa kisiasa usio wa kawaida juu ya mustakabali wake.
Haijawa wazi ikiwa Johnson atabaki ofisini wakati chama cha Conservative kikichagua kiongozi mpya ambaye atachukua nafasi yake kama waziri mkuu.
Afisa mmoja kutoka ofisi ya Johnson ya Downing Street amethibitisha kuwa waziri huyo mkuu atatangaza kujiuzulu kwake baadaye hii leo.
Afisa huyo alizungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwasababu bado hatua hiyo ya kujiuzulu haijatangazwa rasmi.
Wakati huohuo, chama kikuu cha upinzani cha Labour nchini Uingereza, kimesema kuwa matarajio ya kujizulu kwa Johnson kama waziri mkuu ni habari njema.
Lakini mbunge wa chama hicho Keir Starmer ameongeza kuwa kubadilisha kiongozi wa chama cha kihafidhina hakutoshi na kwamba wanahitaji mabadiliko yanayofaa ya serikali.
Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Abdu Mtullya mchambuzi wa masuala ya kimataifa kufahamu kile kilichomsukuma kiongozi huyo kuachia ngazi baada ya kukataa miito ya kujiuzulu na kusema ataendelea kusimama imara katika kuiongoza nchi yake.
#Dwkiswahili

Post a Comment