Balozi
wa Tanzania Nchini Brazili Mhe. Prof. Adelarous Kilangi, amewataka Watanzania
kuzitumia fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini Brazili, hasa kwenye Sekta za
Kilimo, Biashara, Uwekezaji na Mifugo.
Balozi
Kilangi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Vyombo vya habari kwa njia ya
Mtandao wa Zoom, kutokea nchini Brazili ambapo alitumia fursa hiyo kueleza
matunda ambayo Tanzania inaweza kuyapata kupitia ushirikiano wake na Brazili.
"Miongoni
mwa fursa ziliopo Brazili ni kwenye Sekta ya Kilimo hasa kilimo cha Maharage ya
Soya, Mtama na Mahindi ya Njano, kuna kampuni tumewasiliana nayo kutoka China
imekuja Tanzania, imeanza kulima Soya na tunatarajia itaanza kulima Maharage ya
Njano na Mtama, kwa hiyo Wakulima wetu Tanzania wanaweza kuanza kulima mazao
haya." Amesema Balozi Prof. Kilangi
Kuhusiana
na suala kukabiliana na Upandaji wa gharama za Mafuta na nishati Mhe. Balozi
Kilangi amewashauri Wadau wa kujikita zaidi kwenye uzalishaji wa Gesi aina
Ethanol ambayo imesaidia kupunguza gharama ya bei ya mafuta Brazili.
"Kwenye Mafuta na Gesi Ubalozi tulitembelea kiwanda kikubwa cha kuzalisha ETHANOL hapa Brazili, watawekeza Tanzania, tunashauri wadau waitumie fursa hii ya kuzalisha Ethanol, kwa sababu wakati Dunia nzima mafuta yakiwa yamepanda Brazili Petroli inauzwa kwa bei ya chini na sababu kubwa ni wenzetu waliongeza uzalishaji kwenye Ethanol" Ameongeza Balozi Prof. Kilangi

Post a Comment