Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Imelezwa kuwa ili kuongeza idadi ya wanawake wanaoshika ngazi za juu katika uongozi, benki ya KCB Tanzania imejipanga kuwawezesha waajiri wake hususan wanawake kupata mafunzo ya uongozi.
Hilo limeelezwa katika mahafali ya pili ya mpango wa kuendeleza viongozi wa kada ya juu katika taasisi za umma na binafsi unaofanyika chini ya Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEOrt).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa KCB Tanzania Cosmas Kimario amesema wanaamini ili mtu aweze kupata mafanikio ikiwemo katika biashara ni lazima kuwekeza katika uongozi.
Amesema wameweka kipaumbele katika jinsia kwa sababu wanataka kupata viongozi wengi wanawake.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya sheria na Katibu wa bank KCB Atonia Kirama ambaye ni amehitimu mafunzo hayo amesema mafunzo hayo hayatamsaidia kuhudumia wateje wao kwa weledi na kuwongoza vyema wafanyakazi wenzake





Post a Comment