DIWANI CUP KIPAWA KUTOA AJIRA KWA VIJANA




.............................

Na Heri Shaaban (Ilala )


MASHINDANO ya kugombea kombe la IDANI KWEZI Kata ya Kipawa Wilayani Ilala imetoa ajira kwa vijana wanaoshiriki mashindano hayo ambayo awali yalishirikisha timu 32 za Kata ya kipawa

Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Ilala Diwani wa Kata ya Kipawa IDANI KWEZI  alisema mashindano hayo  ni sehemu ya ajira kwa vijana zawadi nono kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu .

Diwani AIDANI alisema zawadi nono zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu Ili vijana waweze kutafuta fursa michezo pia ni sehemu ya ajira na kujenga mahusiano .

" Mashindano ya AIDAN Cup, mshindi wa kwanza kuondoka na kitita cha shilingi milioni 2  tasilimu wakati mshindi wa pili kuchukua kitita Cha milioni 1.5 na wa tatu shilingi 500,000/= timu Bora kikundi Bora zawadi maalum na kikundi Cha Hamasa watazawadiwa shilingi 200,000/= mfungaji Bora kiatu alisema Kwezi .

Diwani AIDANI alisema michezo ni furaha pia ni ajira kwa vijana dhumuni la michezo hiyo kuwaweka vijana pamoja waweze kujiajiri wajiepushe kushiriki katika makundi yasiofaa ikiwemo  madawa ya kulevya .

Alisema mashindano hayo yamefikia hatua ya robo fainali awali kulikuwa na Mtoano timu 40 zikapatikana 16 za Mwaka 2023 wakachanganya na timu 16 za Mwaka Jana jumla zikawa 32 kukawa na atua ya makundi mtoano Mpaka Sasa zimebaki timu nane.

Mwisho

0/Post a Comment/Comments