WAZAZI,WALEZI KUWAJIBISHWA KISHERIA SUALA LA WATOTO WA MITAAN

 Waziri wa Maendeleo  ya Jamii, Jinsia , Wanawake  na Makundi  maalum  Dkt . Doroth  Gwajima akizungumza katika mkutano  wa  siku  mbili uliuowakutanisha   wadau  wa  huduma  za Ustawi   wa  Jamii nchini kwenye ukumbi wa Kizenga Makumbusho jijini Dar es Salaam leo Septemba 6,2022.Waziri wa Maendeleo  ya Jamii, Jinsia , Wanawake  na Makundi  maalum  Dkt . Doroth  Gwajima akizindua mwongozo wa malezi ya watoto na Katibu Mkuu wa Wizara  wa Maendeleo  ya Jamii, Jinsia , Wanawake  na Makundi  maalum Dk. Zainab  Chaula na Mkuu wa Mkoa  wa  Dar   es Salaam   Amos  Makalla.Mkuu wa Mkoa  wa  Dar   es Salaam   Amos  Makalla akizungumza katika mkutano huo wa wadau.

...........................................

NA  SALIM  BITCHUKA 

Waziri wa Maendeleo  ya Jamii, Jinsia , Wanawake  na Makundi  maalum  Dkt . Doroth  Gwajima ameahidi   kuwachukulia  hatua  kali   za  kisheria   wazazi  na  walezi   wote   watakaobainika  kuwaachia   watoto  kuondoka    nyumbani  na   kuingia   mitaani  na  kufanya   shughuli  mbalimbali .

Waziri  Dkt  Doroth   Gwajima   ameyasema   hayo  leo  jijini  Dar es  Salaam   wakati  akifungua   mkutano  wa  siku  mbili uliuowakutanisha   wadau  wa  huduma  za Ustawi   wa  Jamii nchini.

Katika  mkutano   huo  Dkt.  Gwajima  amesema  serikali   ya  awamu   ya  Sita  kupitia   wizara   ya  Maendeleo  ya   Jamii, Jinsia,  Wanawake  na  Makundi   Maalum  kwa   kuungana   na  wadau   wote   wa  ustawi  wa   jamii   wanakuja  na   mpango  maalum  utakaofanikisha  kuondoa   mtandao  mzima unaofanikisha  kuzagaa   kwa  watoto  mitaani  katika   miji  mbali mbali  hapa   nchini .

"Kifungu cha 8 na 9 cha Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, kinampa majukumu mzazi na mlezi kuwajibika katika matunzo, malezi na ulinzi kwa mtoto hivyo  kifungo hicho kinatoa adhabu ya shilingi milioni tano (5)  au kifungo cha miezi isiyozidi sita au vyote kwa pamoja kwa mzazi/mlezi atakayekiuka sheria hii" amesema Mhe. Dkt. Gwajima.

Aidha   waziri   huyo   pia  amesema    wizara   yake  imeona   kuna   umuhimu   wa  kutungwa  kwa  sheria   maalum  itakayo  komesha  vitendo   vya   baadhi   ya  watu  wenye  ulemavu   wanaotuimia   viti   vyenye   magurudumu   kutumia   ulemavu   wao   kwa  kuomba omba   kitendo   alichosema  kinaongeza  kundi   la  Ombaomba  mitaani.

Kwa  upande  wake  Mkuu   wa   Mkoa  wa  Dar   es Salaam   Amos  Makalla akizungumza  katika  mkutano  huo  amesema   kwa  kushirikiana   na   wizara   ya  Maendeleo   ya  Jamii, Jinsia, wanawake  na  Makundi   Maalum  tayari   wanampango kazi   la  kuwajengea   mazingira  mazuri  ya  kuwatambua watoto  wa  mitaani  na  omba omba  kwa   kuangalia  mahala   watakapopelekwa  mara  baada  ya  kuondolewa  mitaani.

Mkutano  huo  wa   wadau wa huduma   za  Ustawi   wa Jamii umekwenda  sambamba  na  uzinduzi   wa   vitabu   viwili  ikiwemo  kitabu   cha   Kanuni  za  Maadili  ya   kufanya  kazi   na watoto pamoja  na  uzinduzi  wa kitabu  cha  kiongozi  cha  penzi  kitakachosaidia   kutoa   muongozo  katika  vituo vya  kulelea  watoto  mchana .

0/Post a Comment/Comments