NA SALIM BITCHUKA,DAR ES SALAAM
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imeielekeza
Serikali kutazama hali halisi na kuchukua
hatua stahiki kuhusu ushauri na maoni ya
wananchi kuhusu Tozo za miamala ya
Kieletroniki, iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni.
Kauli hiyo
imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi Shaka
Hamdu Shaka wakati akiwasilisha taarifa
kwa wanahabari yale yaliyopokelewa na kujadiliwa
katika kikao maalum cha Kamati hiyo
kilichoketi Septemba saba mwaka huu 2022.
Shaka Hamdu Shaka
amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea,
kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea
kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbali mbali ya
maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya kujipatia
maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.
Aidha Kamati Kuu imempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kwa
namna anavyoimarisha huduma za kijamii, kuimarisha ustawi wa wananchi,
kukuza uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele
katika Sekta ya Kilimo kwa kutenga bajeti ya kiasi cha shilingi
bilioni 954 ikiwa ni ongezeko la asilimia 224% .
Sanjari na hayo Katibu huyo wa
Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa ametumia nafasi hiyo kuwataka watendaji wote wa Serikali
kushuka chini na kuhakikisha wanasiliza Kero za wananchi na kuzitatua kwani serikali ya awamu ya
sita haitokubali kuwa na watendaji amabao
hawajui majukumu yao.
Aidha, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
imepokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti
zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbali
mbali ya maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya
kujipatia maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka
2020-2025.
Eneo moja wapo ikiwa ni kupitia Tozo ambapo ni
ukweli usiopingika kwamba serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi
kifupi kwa mfano; kama vile ujenzi wa vituo vya afya 234 na shule mpya za
sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa ambayo yanagusa maisha ya watanzania ya
kila siku.
Hata
hivyo baada ya kutafakari na kujadiliana kwa kina Kamati Kuu imeona
umuhimu wa serikali kusikiliza maoni na ushauri wa wananchi kuhusu utekelezaji
wa bajeti hiyo, hususani katika eneo la Tozo za miamala ya kielektroniki,
iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni.
“Kuongeza
upatikanaji wa huduma za kifedha kwa gharama nafuu kwa kupanua wigo wa matumizi
ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kifedha ili kuongeza huduma jumuishi za
fedha nchini, kuchochea uwekezaji wa ndani na kukidhi mahitaji halisi ya
wananchi hususan wa kipato cha chini na waishio vijijini.”amesema Shaka Hamdu
Kamati Kuu ya CCM imeelekeza Serikali kufikiria na kujielekeza katika kubana matumizi Serikali, kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya kodi ili kuwa na viwango pamoja na mfumo rafiki wa kodi kwa kila mmoja.

Post a Comment