Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto akizungumza na Wakazi wa Ilala Kata ya Mchikichini wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha kisasa kitakacho jengwa ghorofa nne fedha za Tozo za Serikali (kushoto)Diwani wa Kata ya Mchikichini Azim Khan na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji Amani Mafuru.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ilala Mchikichini wakati wa kumkabidhi Mkabidhi mkataba Kampuni ya Ujenzi itakayojenga Kituo Cha Afya Cha kisasa kitakachotoa huduma Ilala yote mkataba huo umeshudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu LUDIGIJA.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto (Kulia wa kwanza)na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Amani Mafuru wakimkabidhi mkataba Mkurugenzi wa Hamfery Construction Ltd Kwa ajili ya Ujenzi wa kituo Cha Afya Cha kisasa gorofa nne Kata ya Mchikichini Septemba 27/2022 (NA HERI SHAABAN ILALA)
...................
Na Heri Shaaban (Ilala )
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 kwa ajili ya kituo cha Afya Wilayani Ilala kinachojengwa Kata ya Mchikichini.
Meya Kumbilamoto alisema ujenzi wa Kituo hicho cha Afya cha kisasa Kata ya Mchikichini kitakuwa mkombozi kwa Wakazi wa Kata ya Ilala ,Mchikichini na kariakoo ambapo hakuna Zahanati wala kituo cha Afya .
Akisaini Mkataba Leo wakati wa ujenzi wa Kituo hicho cha kisasa Kata ya Mchikichini na kushudiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,Mkuu wa Wilaya Ilala Arch,Ng'wilabuzu Ludigija ,Diwani wa Kata ya Mchikichini Azim Khan na viongozi wa CCM kata hiyo ujenzi wa gholofa nne utakaochukua miezi Kumi na mbili.
Meya Kumbilamoto alimpongeza Rais kwa kufuata machozi kilio cha wakazi wa Mchikichini ,Ilala na Kariakoo ambao hawana Zahanati wala kituo cha Afya hivyo ujenzi wa kituo hicho kikubwa gholofa nne kitakuwa mkombozi wao.
"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa kumshawishi Rais Samia kutoa fedha za tozo katika ujenzi wa Kituo hichi cha Afya naomba wananchi wa Mchikichini simamieni mradi wenu huu" alisema Kumbilamoto .
Meya Kumbilamoto alisema wakazi wa Mchikichini ,Ilala na Kariakoo walikuwa wanatabika kukosa Huduma za Afya karibu na Eneo lao kwa Sasa watapata huduma katika kituo hicho na wagonjwa wa Rufaa ndio wataelezwa Hospitali ya Mkoa Amana .
Aidha aliwataka wakazi wa eneo hilo wapewe Vibarua na tenda mbalimbali Ili wajikwamue kiuchumi .
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu alisema ujenzi wa Mradi huo wa Kituo cha Afya Mchikichini ni fedha za ndani za walipa kodi zinatokana na fedha za Tozo .
Mbunge Zungu alisema wenyewe Watanzania tunaweza tulipe kodi pamoja kudai lisiti wakati wa kununua bidhaa Ili kuiongezea mapato Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Naibu Spika Zungu alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mradi mkubwa wa Wilaya ya Ilala ambao unajengwa kwa fedha za Serikali .
Alitumia nafasi hiyo kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan aje kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wake
Aliwapongeza Diwani wa Mchikichini Azim Khan ,Viongozi wa Kata na Matawi na shida kwa uzalendo wao kufanikisha kupatikana eneo hilo
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt.Eldhabeth Nyema, alisema kituo hicho cha Afya ni cha mfano kitatoa huduma nyingi wagonjwa wa nje vyumba sita na vyumba vya madaktari.
Dkt Elidhabeth Alisema kituo hicho Cha Afya kitatoa huduma za Mama na Mtoto na wagonjwa njiti ,wakiwepo na madaktari Bingwa watakaoungana na madaktari wa Hospitali kubwa katika kutoa huduma .
Alisema kituo hicho ni cha mkakati kitaanza kutoa huduma kabla ujenzi wake kukamilika



Post a Comment