MIGOGORO 391 YA ARDHI YASIKILIZWA KWA SIKU SABA


 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepokea  malalamiko 391 kutoka kwa wananchi wa Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam na hoja tatu kutoka Mkoa wa Pwani katika Wilaya za Kibaha na Kisarawe.

Hayo yamesemwa na Katibu MKuu wa Wizara Ardhi  Dkt Allan Kijazi, Leo jijini Dar es salaam,amesema aliunda timu ya Watalaanu kutoka Makao makuu ya wizara kwaajili ya kusikiliza migogoro ya Ardhi kwenye Mkoa wa Dar es salaam kwenye kipindi Cha wiki Moja kuanzai Tarehe 1 ya mwenzi 8 mpaka Tarehe 5.

" Temeke yalikuwepo malalamiko 41 kinondoni 144,

kigamboni 39, ubongo 86, ilala 78, kibaha na kisarawe malalamiko 3 ukijumilisha haya unapata malalamiko 391" amsema Allan Kijazi 

Pia Amesema  kamati ambayo aliunda  ilifanya uchambuzi  wa   kina na  kubaini   Changamoto ambazo  zinahitaji kikao Cha usuluhishi,    ufunguaji   wa mipaka,  Madai ya Fidia, upangaji na umilikishaji.

Katibu MKuu Kijazi Amesema Miongoni mwa kazi zilizofanyika ni ukaguzi wa maeneo 36 kati ya 38 yenye changamato za uvamizi, upimaji na kubainisha mipaka. 

"Wananchi 191 wamepewa majibu kwa kuandikiwa barua kuhusu uamuzi au hatua zinazopaswa kuchukuliwa" amsema Kijazi.

Aidha amsema Kamati imebaini uwepo wa changamoto kwenye maeneo mahususi 

yenye migogoro ya muda mrefu mathalan Mradi wa Kwembe na Eneo la Kitalu ‘E” Goba Manispaa ya Ubungo. 

Amsema Zoezi la kutatua migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam ni endelevu ili 

kuhakikisha maamuzi kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa imefikia mwisho.

0/Post a Comment/Comments