ROYAL TOUR YA TZ KUJADILIWA KWENYE MKUTANO WA 51 GENEVA USWISI.


........................

Ujumbe kutoka  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka umehudhuria mkutano  Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu  unaendelea  Geneva, Uswisi.

Katika  mkutano  huo  Ujumbe   wa Tanzania  imejipanga  kuzungumzia  Ajenda  ya  haki  ya  Maendeleo  kwenye   Elimu , Afya, Makazi,Maji Salama na  Safi .

Pia  Ujumbe utaongelea pia athari za Uviko 19 hasa katika sekta ya Utalii  na mikakati madhubuti iliyowekwa ya kudhibiti uchumi dhidi ya janga la Kovid 19, ikiwemo kuhimiza  utoaji wa chanjo ya uviko na kutangaza Nchi kupitia Royal Tour, ambayo imeleta matokeo chanya  yaliyopelekea  watalii kuongezeka kwa kiwango kikubwa mbali  na  Ajenda  hizo  pia  kutakuwa  na vikao vya  pembeni.

Mkutano  huo wa 51 wa  Baraza la  Haki  za Binadamu Umeanza tarehe 12 Septemba na utaendelea hadi tarehe 7 Oktoba 2022 mbali  na  ujumbe  huo  pia  tunawakilishwa Balozi Maimuna Tarishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva.

0/Post a Comment/Comments