SERIKALI KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA WAANDISHI BUNIFU

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Taifa Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu iliyofanyika leo Septemba 12,2022 katika ofisi za Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizindua Tuzo ya Taifa Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu leo Septemba 12,2022 katika ofisi za Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam 

..............................

NA SALYM BITCHUKA,DAR ES SALAAM

Serikali  kupitia  Wizara   ya  Elimu  Sayansi  na  Teknolojia   imeahidi  kufufua   hali   Uandishi , Uchapaji, Uchapishaji ,Usambazaji   na  usomaji   wa  vitabu  hasa  kazi  za  waaandishi  Bunifu.

Kauli  hiyo  imetoleewa  leo jijini  Dar  es Salaam na  waziri  wa  Elimu Sayansi  na Teknolojia  Profesa  Adolf  Mkenda  wakati   wa  uzinduazi  wa  Tuzo  ya  Mwalimu  Nyerere  ya  Uandishi   Bunifu.

Waziri   Profesa   Mkenda  amesema  ili  kuweza  kuchochea  na  kufanikisha   Uandishi,  Uchapishaji  na  Usomaji ,   wizara imeahidi   kupita   bajeti  ijayo  itatenga  fedha  kwa ajili  ya  kununua  na  kuvisambaza  vitabu  vya  ithibati  ili viwezwe  kusomwa   na  kuleta  hamasa.

Akizungumza  katika  uzinduzi  huo  Mkurugenzi  Mkuu  Taasisi  ya Elimu  Tanzania ( TET ) Dkt.  Aneth  Komba  amesema  lengo  la  tuzo  hiyo  ni kukuza  sekta  ya  uandishi  na  uchapaji  nchini  na  kuongeza   hari  ya  Watanzania  kujisomea  huku Mwenyekiti  wa  Kamati ya Tuzo  ya  Taifa ya Uandishi  Bunifu  Profesa  Penina  Mlama  akisema  jamii  yoyote  ilyostarabika huthamini  waandishi  Bunifu  huku akibainisha  kuwa Uandishi  Bunifu  imetoa mchango  mkubwa  katika  kukuza Lugha ya  Kiswahili  Duniani.

Imeelezwa kuwa  kuanzishwa  kwa  Tuzo  hiyo   ya  Taifa  ya  Mwalimu  Nyerere   ya  Uandishi  Bunifu   ya  Taifa  ni  muhimu  kwa  maendeleo  ya  nchi ikienda  sambamba  na kuwatambua  kitaifa  na  kuzawadiwa  kwa  waandishi  mahiri  wa  uandishi  Bunifu katika  nyanja  za  riwaya  na Ushairi  kwa kuanzia  huku  ikiwa na  lengo  la  kukuza  utamadunu  wa  Tanzania  kujisomea  na  kuhifadhi  historia, amali  na mitazamo bora  ya  watanzania.

Aidha amesema majaji watapitia maandiko ya kila mshiriki atakayetuma kupitia barua pepe na Zawadi nono Kwa washindi itakuwepo ambapo mshindi wa kwanza atapewa kiasi cha shilingi milioni 10 huku wa pili akipatiwa shilingi milioni 7 na watatu atapewa milioni 5 hivyo Waandishi wote wa vitabu andikeni kazi nzuri na hii itakuwa kila

0/Post a Comment/Comments