....................................................
Serikali imejipanga kufunga Rada saba katika maeneo mbalimbali nchini ili kuisadia Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini- TMA kuendelea kufanya kazi zake kwa ufanisi katika utabiri wa hali ya hewa.
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika Kongamano la 15 la wadau wa Satelite za hali ya Hewa za Shirika la EUMETSAT Barani Afrika ambao unafanyika kwa siku tatu ambapo takriban Nchi 50 kutoka Afrika wameshiriki katika kongamano hilo la watumiaji wa taarifa kutoka kwenye satelaiti za Hali ya Hewa ili kuangalia faida wanazozipata kutoka katika satellite hizo.
Akizungumza katika Kongamano hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema Serikali itaendelea kufunga rada katika maeneo mbalimbali ili kufanya urahisi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Naibu Waziri ameipongeza serikali kwa kuendelea kuongeza rada zitakazosaidia katika ufanisi wa TMA kwa kutoa taarifa kwa wakati za Hali ya Hewa na hivyo kuwafanya wananchi kuufahamu umuhimu wa Utabiri ulio sahihi.
Aidha amesema kuwa serikali itakwenda kufunga rada katika mikoa mbalimbali hasa ya Nyanda za Juu kusini ukiwemo Mkoa wa Kigoma lakini pia rada nyingine zipo kwenye matengenezo na zitakapokamilika zitafungwa.
‘Rada tatu zimefungwa tayari na mbili zimekamilika tutaanza kufunga wakati wowote kuanzia sasa lakini pia mbili zipo kiwandani kwenye matengenezo na zote Mhe Rais ameshalipa fedha’amesema Naibu Waziri Mwakibete
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt Agnes Kijazi amesema katika mkutano huo pia wanaangalia faida na changamoto zilizopo ili waweze kuziboresha.
Ameeeleza kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo ni heshima kubwa kwa nchi na kuonesha mafanikio makubwa katika sekta ya hali ya hewa nchini pamoja na ushirikiano ulipo baina ya nchi za Afrika na nje ya Afrika.
Amesema kuwa Sateline inaona kutoka angani na kuangalia maeneo yote ya nchi hivyo inatoa msaada mkubwa kwa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya kutoa utabiri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EUMETSAT, Dkt. Phil Evans amesema mipango ya shirika hilo ni kurusha satelaiti ya kisasa zaidi (Meteosat third Generation – MTG) mwishoni mwa mwaka huu ili kuboresha uangazi na utoaji wa taarifa za hali ya hewa hususani katika ukanda wa Afrika.
Imeelezwa kuwa Kongamano hilo wadau wa Satelite za hali ya Hewa za Shirika la EUMETSAT Barani Afrika ambalo kauli mbiuy yake mwaka huu ni ‘Kuelekea kizazi kipya cha Sateliti za hali ya hewa kwa Afrika’hufanyika kila baada ya miaka miwili na uliahirishwa kufanyika mwaka 2020 kutokana na janga la UVIKO-19 ambalo lilikuwa limeikumba dunia.




Post a Comment