Kamishna wa Elimu nchini Dkt Lyabwene Mtahabwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Ripoti ya utafiti uliofanywa na Asasi ya HakiElimu Mwaka 2022 kuhusu mchango wa Elimu ya uraia Shule za Sekondari na ushiriki wa vijana katika michakato ya kidemokrasia nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HakiElimu Godfrey Boniventure katika uzinduzi wa Ripoti ya utafiti uliofanywa na Asasi ya HakiElimu Mwaka 2022 kuhusu mchango wa Elimu ya uraia Shule za Sekondari na ushiriki wa vijana katika michakato ya kidemokrasia nchini.
Mwalimu wa Shule ya Jangwani Sekondari anayefundish somo la Uraia
Fransiska Njagira akielezqa namna wanavyowafundisha wanafunzi masomo ya uraia.(picha
na Mussa Khalid)
................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Imeelezwa kuwa sehemu kubwa ya jamii bado inashindwa kuoanisha elimu uraia na Maandalizi ya viongozi na siasa safi hali inayochangia kutoa hamasa kidogo kwa vijana kushiriki katika shughuli za siasa na Demokrasia wakiwa bado shuleni.
Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Ripoti ya utafiti uliofanywa na Asasi ya HakiElimu Mwaka 2022 kuhusu mchango wa Elimu ya uraia Shule za Sekondari na ushiriki wa vijana katika michakato ya kidemokrasia nchini ambapo katika ngazi ya shule umeonyesha asilimia 44.4 ya wanafunzi hawaelewi maana ya Demokrasia.
Akizungumza katika hafla Hiyo Kamishna wa Elimu nchini Dkt Lyabwene
Mtahabwa amesema kuwa Demokrasia ni vyema ikajengwa juu ya msingi wa uzalendo
ili kuweza kuyafanikisha yale ambayo Taifa linahitaji katika kupata
kizazi kilichobora cha baadae.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HaliElimu Godfrey Boniventure amesema kuwa Shirika hilo kwa sasa linajikita katika utekelezaji wa mradi wa kukuza ushiriki wa vijana kenye Demokrasia.
Amesema kabla ya kutekeleza mradi huo wameanza kufanya utafiti wa kina ili kufahamu hali ya ushiriki wa vijana katika ngazi ya Demokrasia kwani ndio eneo ambalo ni muhimu zaidi katika kushiriki kwenye fursa mbalimbali za kufanya maamuzi.
Aidha amesema katika ufanyaji wa tafiti hiyo wamebaini changamoto ambazo zipo kwenye mtaala likiwemo Neno Demokrasia maana yake halijitoshelezi kwa sababu linajikita katika maeneo Fulani badala ya kueleza kwa upana.
‘Kwa mfano wanafunzi wengi ambao wamekuwa wakiulizwa wanajibu kwamba ni masuala yanayohusiana na uchaguzi kitu ambacho kinaleta changamoto ya namna ya kutoa elimu ya uraia’ amesema Boniventure
Mtafiti aliyeshiriki katika Utafiti huo Pepetua Kalimasi amesema asilimia 68.9 hawajawahi kugombea na kuonesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ngazi ya shule huku Mwalimu wa Shule ya Jangwani Sekondari anayefundish somo la Uraia Fransiska Njagira amesema wanafunzi wamekuwa wakionyesha jitihada za kuwashirikisha wanafunzi katika chaguzi mbalimbali.
Kwa mujibu wa utafiti huo umebaini vijana wanatarajia kuwa shule ndio chanzo kikuu cha kujifunza na kujengewa uzoefu katika michakato ya kidemokrasia na kusikiliza kwenye vyombo vya habari na kujisomea kwenye mitandao ya kijamii na vitabu.
Katika ngazi ya jamii utafiti huo umeishauri mamlaka kuhakikisha wanatoa
fursa kwa vijana kushiriki katika shughuli mbalimbali za siasa na demokrasia
katika ngazi za vijiji au mitaa.
Post a Comment