Na
Mwandishi wetu.
Waziri
Mkuu wa Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter
Pinda ameagiza Makumbusho ya Taifa la Tanzania kuendelea kutangaza vivutio
vya Makumbusho na malikale kwa faida ya
kizazi cha sasa na kijacho.
Mhe. Pinda aliyasema hayo alipotembelea Kijiji cha
Makumbusho kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam akiambatana na mkewe Bi
Tunu Pinda.
Amesema
Makumbusho ya Taifa inatakiwa kuendelea kuweka mikakati ya kutangaza vivutio
vya Makumbusho na malikale ili kukuza utalii nchini.
“Tuendelee
kuweka mikakati zaidi katika kuitangaza Makumbusho na vivutio vyake kwa lengo
la kukuza Utalii na hasa kwa kizazi kilichopo na kijacho”. alisema Mhe. Pinda
Mhe.
Pinda alipata nafasi ya kujua historia na tamaduni za Makabila 120 ya Tanzania
kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho Bi Agnes Robert.
Akiwa
Kijiji hapo alipata nafasi ya kukutana na
watalii wengine kutokea nchini
China ambao walikuja kutalii Kijiji cha Makumbusho na kujifunza historia ya
Makabila ya Tanzania na teknolojia ya ujenzi wa nyumba za asili.
Mhe
Pinda alifurahia kukutana na watalii hao kutoka China na kuzungumza nao kuhusu
walichojifunza walipotembelea Kijiji cha Makumbusho.
Vile
vile alipata nafasi ya kukutana na watoto wa shule ya msingi Gifted Kids,
waliokuja kufanya utalii Kijijini hapo kujifunza utamaduni unaohifadhiwa hapo.
“Nimefurahia
kuwaona watoto wadogo wakicheza ngoma za asili kwani hivi ndivyo inatakiwa
maana watoto wanaona na kufanya kwa vitendo hivyo hawezi kusahau”. alisema Mhe.
Pinda
Mwisho
alipata nafasi ya kuwatembelea wajasiriamali waliopo Kijiji cha makumbusho na
kutoa ushauri kwa uongozi wa Makumbusho
ya Taifa kuangalie jinsi ya kutangaza kazi hizi za sanaa za mikono kwani ni
moja ya kivutio kwa watalii.
' Makumbusho ya Taifa iangalie jinsi ya kutangazaa bidhaa hizi maana ni sehemu ya utalii' alisema Mhe. Pinda

.jpeg)

Post a Comment