UNYANYASAJI , NGONO NA MIKATABA HEWA YA AJIRA VYATAJWA KWENYE RIPOTI YA LHRC 2022


............................

NA SALYM BITCHUKA

Ripoti ya haki za Biashara na Binadamu 2021- 2022 imeonyesha kuwa bado kumekuwepo na kuongezeka kwa vitendo vya unyanyasaji mahali pa Kazi , changamoto za Haki za Wafanyakazi katika masuala ya mikataba ya Ajira kwa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuminywa kwa kuanzishwa kwa vyama vya wafanyakazi nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar e Salaam na Mkurungezi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) Wakili Anna Henga amesema kwa sasa matendo hayo ya unyanyasaji mahala pa kazi yameongezeka kwa asilimia mbili kwani katika tafiti zilizopita ilikuwa ni aslimia 31 na kwa tafiti za mwaka huu ni asilimia 34.

Aidha Wakili Anna Henga amesema kupitia tafiti za ripoti hiyo katika masula ya haki za wafanyakazi katika mikataba ya Ajira bado kumekuwepo na changamoto japo kwa mwaka huu ikiongezeka kwa asilimia nne kutoka alimia 48 hadi asilimia 52.

Kwa upande wake Mtafiti wa Ripoti ambye ni Afisa Progam Mwandamizi Maswala ya Biashara na Haki za Binadamu kutoka Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC) Joyce Komanya amesema kukosekana Kwa Sheria Maalum ya haki za binadamu na biashara kunachangia wafanyakazi hasa katika sekta binafsi kukosa stahiki zao ikiweemo mishahara, likizo ,Pesa za ziada na likizo ya uzazi,

Sanjari na hayo kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC )Kimetoa rai kwa waajiri kuangalia suala la haki za wafanyakazi haswa katika muda wa kazi ili wasifanye kazi kupita kiasi kwa kuwa ni athari katika mazingira ya kazi .

Ripoti hiyo iliyozinduliwa leo na LHRC imelenga kuyakumbusha makampuni na wafanyakazi nchini kuheshimu haki za Binadamu katika utekelezaji wa shughuli zake na kuikumbusha Serikali kulinda haki za wafanya kazi na wanajamii ambao wanaweza kuathirika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za Binadamu vinavyofanywa na Makampuni. 

0/Post a Comment/Comments