
Baadhi ya wavuvi wakiendela na shughuli zao za uvuvi
........................
NA MUSSA KHALID
Wavuvi nchini wameiomba Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini–TMA kuendelea kutoa tabiri zinazowasaidia wafanye kazi zao za uvuvi kwa ufanisi ili waweze kuchukua tahadhari za upepo mkali ukiwemo wa Matlai.
Wameeleza hayo leo jijni Dar es salaam wakati wakifanya mahojiano na kituo hiki kuhusu utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na TMA unawasaidiaje katika shughuli zao za uvuvi wakiwa baharini.
Wavuvi Abduli Alexi pamoja na Faraja Faraja wamesema changamoto ambayo wamekuwa wakikumbana nayo katika shughuli za uvuvi ni pamoja upepo mkali ambao kujitokeza mara kwa mara na hivyo kukwamisha shughuli zao.
Aidha wameipongeza TMA Kwa kuendelea kutoa taarifa za mara kwa mara ambazo zinawasaidia katika kufanya Kazi zao kwa tahadhari na hivyo kuepukana na madhara.
Kuhusu uwepo wa upepo wa Matlai Kaskazini,Meneja wa Kituo kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa–TMA Samweli Mbuya amesema kuwa upepo huo umekuwa ukiashiri muelekeo wa msimu wa mvua za vuli.
"Kiujumla upepo huu unatoka Mashariki Katika bahari ya Hindi kuelekea Katika maeneo ya nchi yetu na Matlai ya Kaskazini unaambatana na kipindi cha msimu wa Vuli na Matlai ya Kusi inaambatana na kipindi cha Msimu wa Mvua za Masika"amesema Mbuya
Mbuya amesema kuwa utakapofika msimu wa Vuli ndio wataanza hasa kuangalia upepo huo kwa makini Pamoja na mwenendo wake kwa sababu utakuwa unaambatana na Mvua ambazo zinakumba maeneo yote yanayopata Mvua za Vuli.
Hivi karibu Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa utabiri wa Mvua za Vuli Oktoba mpaka Disemba mwaka huu na kueleza mvua zinatarajiwa kuwa za wastani ambapo imewashauri wavuvi kufuatilia na kutumia taarifa sahihi za utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na kuzingatia ushauri.


Post a Comment