WUVB, BRELA NA WADAU BIASHARA KUJADILI SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA ZILIZOPITWA NA WAKATI .

Mkurugenzi  wa  leseni   kutoka Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  ( BRELA)  Andrew  Mkapa akifungua kikao cha kujadili kupata  maoni  na   mapendekezo  ya   Mabadiliko   ya   Sheria  ya  leseni  za  Biashara  ya  mwaka  1972


..............

NA SALIM BITCHUKA

Wizara  ya  Uwekezaji, Viwanda  na  Biashara   kwa  kushirikiana  na   Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  ( BRELA) pamoja  na  Taasisi  za  Sekta  za  Umma    wamekutana  ili  kupata  maoni  na   mapendekezo  ya   Mabadiliko   ya   Sheria  ya  leseni  za  Biashara  ya  mwaka  1972.

Akifungua   kikao  hicho  leo Septemba 14,2022  jijini  Dar  es Salaam Mkurugenzi  wa  leseni   kutoka Wakala  wa Usajili  wa   Biashara  na  Leseni  ( BRELA)  Andrew  Mkapa  amesema  kupitia   kikao   hicho  kutawezesha  kupatikana  mchango   utakaofanikisha    maboresho  ama   marekebisho    ya    Sheria  ya  leseni  za  Biashara , Sura  208   ambayo   imeonekana  kupitwa   na  wakati.

Aidha   Andrew  Mkapa  amesema  Sheria  iliyopo  kwa  sasa  haiendani   na  mazingira   ya  wakati  huu  ambapo   imeonekana   kuwepo   na  mikwamo  kadhaa   kutokana   na  Mabadiliko  ya  Teknolojia  ya  Ufanyaji  Biashara  huku  akitolea   mfano   uwepo  wa  Biashara  za  Mitandao.

Kwa   upande  wake  Afisa  Biashara   kutoka  Wizara   ya  Uwekezaji , Viwanda  na  Biashara (WUVB ) Denis  Mzamiru  amesema   kinachowasukuma   kufanya  maboresho  na   Marekebisho  ya  sheria   hiyo   ni   pamoja  na   kuifanya   Sheria  kuendana  na  Mazingira  ya   Sasa   ya  Ufanyaji   Biashara  ikienda  sambamba   na  uwepo   wa  urahisi  na  wepesi   kwa  wafanyabiashara  kupata  leseni  za  Biashara.

Kikao   hicho  cha  Siku  tatu  pia   kitawashirikisha   wafanya biashara   binafsi   kupitia   miavuli  yao  kimeandaliwa  na  Brela   ikiwa   ni  agizo   kutoka   kwa  Waziri  wa  Uwekezaji,Viwanda  na  Biashara Dkt.  Ashatu  Kijaji   kutaka   kuwepo  kwa  mchakato  wa  kuboresha  sheria  ikienda sanjari   na  kushirikishwa  kwa  wadu  wanaoitumia  sheria   hiyo 

0/Post a Comment/Comments