ZAIDI YA WASHIRIKI 70 WENYE MATATIZO YA KUSIKIA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU MAJUKUMU YA MAMLAKA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice  Mafumiko 

...................

NA SALIM  BITCHUKA 

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  nchini  imetoa   mafunzo  kwa  kundi  maalum  la  watu  wenye  matatizo  ya  Kusikia  lengo  likiwa  ni  kuwapa  uelewa  sahihi  namna  bora  ya  matumizi  sahihi  ya  Kemikali.

Akifungua  mafunzo hayo  leo  jijini  Dar  es Salaam  Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice  Mafumiko  amesema  wanatoa   mafunzo  hayo  ili  kuhakikisha  kuwa  kundi  hilo  la  watu   wenye  matatizo  ya  Kusikia   linapata  uelewa  Sahihi  wa huduma   zinazotolewa  na  Mamlaka  ya maabara  ya  Mkemia  mkuu  wa  serikali.

Dkt.  Fedelice   Mafumiko  amesema  pamoja  na  kuwaongezea  uelewa sahihi  pia  mamlaka  imewaeleza  umuhimu wa   Kemikali   pamoja  kueleza   namna   gani  Kemikali   inaweza  kuleta  madahara  kama  haikutumika  vizuri .

Aidha   Mkemi   Mkuu  wa  Serikali  amesema  kwa  kuona  umuhimu  wa  Kundi   hilo  la watu  wenye  matatizo ya kutokusikia kabisa  na  kutokusikia  vizuri  kutoka  Taasisi  ya Maendeleo  kwa  Viziwi  Tanzania  (TAMAVIKA) ameweka  wazi   kuwa   wataweka  utaratibu  mzuri  wa kuwasajili  wale  wote  wanaohusika  na  uzalishaji  ama  kutumika  katika huduma  za  Kemikali  ikiwemo Matumizi.

Kwa  uapnde  wake  Mkurugenzi  wa  Taasisi  ya Maendeleo  kwa  Viziwi  Tanzania  (TAMAVIKA)  Kelvin  Nyema  amesema kupitia  mafunzo  hayo  yatawajengea  uwezo  na  uelewa  mzuri kuhusu  matumizi sahihi ya  Kemikali  huku  akisema  Kemikali   ni  nzuri  kama itatumika  kwa  usahihi  katika  matumizi  sahihi.

Mafunzo   hayo  yametolewa  kwa  watu zaidi  ya  Sitini  wenye  matatizo  ya kutokusikia  kabisa  na  wale  ambao hawasikii vizuri   kutoka  katika   mikoa  ya  Pwani  na  Dar  es Salaam  

0/Post a Comment/Comments