Amesema kuwa Gf Truck Group wanapaswa kupongezwa kwa hatua yao ya kuendesha zoezi hilo kupitia maonyesho hayo ya tano ya teknolojia ya madini nakwamba moja ya jambo ambalo serikali wanalisukuma lifanyike nikuwafanya watanzania washiriki kwenye uchumi wa madini na katika hilo kuna watu wapo kwenye kilimo,Madini,na wengine kwenye mifugo hao wote waone uwepo wa madini ni fursa kwao ili kukuza uchumi wao.
Gf Truck tunawapongeza sana hususani kwa siku yenu ya leo umeonyesha jambo kubwa la kuchangia damu na tunawatakia kila la heri na hapa naomba nitowe wito kwa watanzania wengine tuwe na utaratibu wa kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wezetu."
Nakuongeza kuwa "Gf Truck wameonyesha mfano wa kuigwa na naomba na nitowe anasa kwa kampuni nyingine pamoja na kufanya maonyesho lakini kuna kitu ambacho kinagusa maisha ya watu moja kwa moja hivyo Mungu awabariki asanteni sana."amesema Waziri Biteko
Kwa upande wake Meneja masoko na Mawasiliano wa Kampuni hiyo ya Gf Truck Smart Deus akizungumza mbele ya Waziri Biteko amesema kuwa wameendesha zoezi hilo ikiwa ni kuwarudishia jamii katika kile ambacho wanakipata.
Amesema kuwa anaamini yeye pamoja na kampuni yake jambo ambalo wamelifanya linakwenda kuacha alama kubwa hususani kwa wananchi wa mkoa wa geita.
Kwaupande wake Mshauri wa Damu salama kutoka Hospitali ya rufaa Mkoani humo Halima Juma amesema kuwa tangu kuanza kwa maonyesho hayo Septemba 27 mwaka huu hadi kufikia leo Oktaba mosi wamefanikiwa kukusanya chupa 148 za damu.
Pia katika hatua nyingine Halima kupitia Gf Truck Group Day amesema kuwa watu ambao wamewafikia katika kuchangia Damu Salama ni pamoja na watu wa boda boda,na wasanii na wananchi waliohamasika kupitia Kampuni ya Gf Truck Group ni 75 na kati ya hao waliofanikiwa kuchangia damu ni 25 na 50 waliobaki hawakufanikiwa kutokana na sababu mbalimbali.
"Tunashukuru Gf Truck Group kwa mchango wao kwenye timu ya damu salama na hospitali kwa ujumla kwa kuchangia viburudisho,na tishert kwa wachangiaji wakiwemo watumishi wa Damu salama.



Post a Comment