CHIPSIKA NA COKE YAUNGANA NA M_GAS KUMSHIRIKISHA MKONO MJASIRIAMALI

 


  Muhasibu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Ustawi wa jamii Aisha Kapande akisisitiza kuwa washiriki watapata nafasi ya kupewa mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kutunza Fedha zao pamoja na Afya ya akili katika kutoa Huduma kwa wateja wao.


Meneja Masoko wa Kampuni ya M_Gas Nelson Chusi akizungumza na waandishi wahabari Octoba 11 Mikocheni Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua rasmi Kampeni ya "Chipsika kiajira na Coke" akihaidi kuwapa washindi jiko la gesi lenye kifaa kinachosaidia kiwango cha matumizi ya gesi hiyo.

Meneja Mahusiano kwa umma kutoka Kampuni ya Cocacola Victor Amos akikaribisha wajasiriamali mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya "Chipsika kiajira na Coke" iliyofanyika Mikocheni Jijini Dar es salaam yenye lengo la kuwakwamua kiuchumi wajasiriamali wadogo hususani Vijana wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kuwapatia Vitendea kazi ikiwemo Kabati la chips,Nguo za upishi pamoja na Jiko kutoka M_Gas



Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

KAMPUNI ya Cocacola wazindua rasmi Kampeni ya "Chipsika kiajira na Coke" ambapo Vijana 300 katika wilaya zote za Jijini la Dar es salaam kushikwa Mkono kwa kupatiwa vitendea kazi.

Akizungumza na waandishi wahabari octoba 11 Jijini Dar es salaam,Meneja Mahusiano kwa umma kutoka Kampuni ya Cocacola Victor Amos amesema Kampeni hiyo inalenga kuwashika mkono vijana katika Wilaya za Jijini Dar es salaam ikiwemo Kinondoni,Ilala,Temeke,Kigamboni ili kuboresha biashara zao na kuwapa elimu namna ya kufanya biashara ya chips.

Aidha,Amos ameeleza kuwa kwa sasa Kampeni hiyo Ina lengo la kuwakwamua kiuchumi wajasiriamali hususani vijana wa kitanzania mkoa wa Dar es salaam na kwa sasa Washiriki wanaruhusiwa kutuma maombi ili Kamati ya timu ya Kampeni hiyo kuchunguza vigezo vya kukidhi kushiriki.

"Fomu zinazopatikana ofisini Mikocheni kiwanda cha cocacola, mtandaoni kwenye kurasa za cocacola hivyo washiriki hasa wapishi wa chips wanaruhusiwa kuanzia kushiriki Huku vigezo na masharti kuzingatiwa ikiwemo mshiriki awe kuanzia miaka 18 mpaka 35,awe raia wa Tanzania,awe na vitambulisho vya kiraia."

Pia ameeleza kuwa Shindano hilo linatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu Huku maombi ya ushiriki yakifikia kikomo octoba 26 mwaka huu .

Hata hivyo Kwa upande wa Mdhamini wa Shindano hilo  kutoka Kampuni ya M_Gas Meneja Mauzo na Maendeleo Nelson Chusi amesema Kwa kushirikiana na Cocacola wameamua kuungana nao ili kuwawezesha vijana kuendana Mabadiliko ya nishati ya gesi katika matumizi mbalimbali ikiwemo kupika Ili kutunza Mazingira na kuacha Kabisa matumizi ya mkaa.

"Kupitia huduma ya M_gas inawezesha watumiaji na hata wajasiriamali kujua Salio lililobakia kwenye mtungi pamoja na kununua gesi kwa kima cha chini shilingi elfu 1 kulingana na matumizi yake."

Hata hivyo ameongeza kuwa katika Kampeni hiyo watatoa jiko la gesi pamoja na vifaa vyote kwa washindi wa Kampeni hiyo kama sehemu ya kuunga Mkono na kuwanyanyua vijana kiuchumi Huku Elimu ya namna gani matumizi ya M_gas itakavyotunza vipato vyao kupitia huduma mbalimbali ikiwemo mkopo wa gesi kwa gharama ya shilingi elfu 40.

Pia Kwa upande wa Muhasibu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Ustawi wa jamii Aisha Kapande amesema wajasiriamali watapata nafasi ya kupewa mafunzo ili waweze kuendesha biashara zao huku wakiwa na nidhamu ya kutunza Fedha zao.

"Tukishirikiana na cocacola tunaenda kutoa Elimu kwa washiriki wa "Chipsika kiajira na Coke" ili wawe na biashara itakayokuwa ikikuwa siku Hadi siku pamoja na utunzaji wa kifedha,uwiano wa kibiashara na kuweza kuweka pembeni Matatizo ya Afya ya akili Ili kuepusha uvunjifu wa uaminifu kati ya mteja na muhudumu wake pamoja na swala la usafi wa Mazingira kwenye biashara yake."

Aidha ameongeza kuwa wajasiriamali hao watakaopata nafasi ya kushiriki Mafunzo hayo watafundishwa jinsi ya kumuhudumia mteja wake na kumpa Huduma nzuri .

0/Post a Comment/Comments