FAMILIA YA MTEMVU YAOMBA HAKI ITENDEKE

 




NDUGU wawili wa aliyekuwa Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu, Ibrahim Mtemvu na Jasmine Mtemvu wameomba haki itendeke baada ya kuondolewa kwa nguvu katika nyumba ya urithi ya mama yao wakati kesi kuhusu mgogoro wa nyumba hiyo ikiwa bado mahakamani

Wawili hao ambao shauri lao kuhusu nyumba hiyo likiendelea kusikilizwa katika Kituo Jumuishi cha Haki Temeke, wametoa kauli hiyo jana mara baada ya kundi la watu lililokuwa limeongozana na baadhi ya Askari Polisi kufika katika eneo hilo na kuwamuru kutoka.

Mbali na kuwatoa pia watu hao wamefunga Mgawaha maarufu ya New Didiz na biashara zote zilizokuwepo nje ya nyumba hiyo iliyopo Masaki Mtaa wa Haile Selassie Kitalu Namba 1036/B2 ambayo inadaiwa kuuzwa na ndugu yao Abbas Mtemvu 

Awali Wakili wa walalamikaji hao Adili Kiiza kutoka Kampuni ya 'Girrafe Attoney' hatua hiyo kutoka kwa walalamikaji hao imetokana na kitendo cha ndugu yao huyo 'Abbas' kuiuza nyumba hiyo ya urithi kutoka kwa Mama yao Sitti Kilungo Mtemvu bila kuwashirikisha. 

"Kesi hii ya marejeo ya madai namba 29 tuliyoifungua katika mahakamani hapa imetokana na kesi msingi namba 474 ya mirathi tukidai haki ya wateja wangu ambao wamepokonywa na ndugu yao baada ya kuiuza pasipo kuwepo makubaliano yoyote kati yake na wao" alisema Kiiza

Kimsingi Abbas Mtemvu alitumia mbinu zisizo sahihi kisheria kupata usimamizi wa mirathi katika Mahakama ya Mwanzo ya Temeke, na baada kuidhinishwa kuwa msimamizi wa mirathi hiyo alianza kukusanya na kuuza vitu pamoja na mali mbalimbali za marehemu bila kuwashirikisha ndugu zake.

Alisema kutokana na hatua hiyo ndugu zake hao waliamua kwenda kufungua kesi ya madai katika mahakama hiyo hiyo ya Mwanzo ya Temeke ambapo hata hivyo waligonga mwamba baada ya kuambiwa kuwa shauri la kesi hiyo tayari limeshafungwa.

"Kwa utaratibu wa kisheria ikiwa shauri limeshafungwa kunakuwa hakuna nguvu za kuendelea na kesi, lakini wakati bado tunatafakari hilo, mlalamikiwa alirejea tena katika mahakama hiyo kuitaka itoe amri ya ndugu yake kuondoka katika nyumba aliyoiuza jambo lililotufanya na sisi kupata upenyo wa kufungua madai yeti" alisema Wakili huyo

Alisema walifungua shauri hilo kuitaka Mahakama ya Mwanzo Temeke kufanya marejeo ya shauri la mirathi iliyofunguliwa na Kaka yao(Abbas) lengo ikiwa kupata mwenendo mzima wa shauri lililoendeshwa hadi kupata idhini ya kuwa msimamizi wa miradhi na baadae kuiuza nyumba hiyo.

" Baadae tuliihamishia kesi hiyo katika Mahakama hii Jumuishi ya Temeke ili kuhakikisha haki ya wateja wangu inapatikana, lakini hata hivyo kesi hiyo ya marejeo iliyopaswa kusikilizwa leo(jana) imeharishwa hadi Novemba 13" alisema Kiiza

0/Post a Comment/Comments