NA SALYIM BITCHUKA
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya
kimataifa ya kupinga Adhabu ya kifo, Kituo cha Sheria na haki
za Binadamu LHRC Kimeitaka serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanania kufanya marekebisho ya
sheria ya kanuni ya Adhabu ili kuondoa vifungu vinavyoweka
adhabu ya kifo ili kulinda haki ya kuishi kwa
kuweka adhabu mbadala.
Tamko hilo limetolewa leo Octoba 10, 2022
jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Kituo
cha sheria na haki za Binadamu (LHRC)
Wakili Anna Henga wakati akizungumza na
wanahabari kuhusu maadhimisho ya 20 ya siku ya Kimataifa
ya kupinga adhabu ya kifo.
Wakili Anna Henga amesema Adhabu
ya Kifo ni adhabu inayotweza utu wa
mtu na kuvunja haki ya kuishi kama iliovyoainishwa
katika mikataba ya kimataifa na kikanda ya Haki
za Binadamu.
Aidha Wakili Henga amesema
uwepo wa Adhabu ya Kifo
haufanyi watu waogope kutenda makosa badala yake
inaongeza maumivu kwa jamii hasa
kwa familia za wafiwa.
Takwimu kutoka Mtandao wa kidunia
wa Kupinga Adabu ya Kifo ambapo
LHRC ni Mwanachama zinaonyesha kuwa
kati ya Mataifa 192
Duniani nchi 110 zimefuta Adhabu ya Kifo,
nchi 55 zinaadhabu ya Kifo kati ya hizo nchi 27 zimekuwa haitekelezeki adhabu hiyo.
Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo huadhimishwa kila ifikapo Octoba 10 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu yana kauli mbiu isemayo “ Adhabu ya Kifo barabara iliyojaa Mateso “

Post a Comment