NHC YATANGAZA KAMPENI YA WADAIWA SUGU

 

Muungano Saguya Meneja habari na Mawasiliano Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wadaiwa sugu wa shirika hilo ambapo kampeni maalum ya kukusanya madeni itaanza hivi karibuni kulia ni Elias Msese Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Miliki (NHC) na kushoto ni Levinico Mbilinyi Meneja wa Kukusanya madeni (NHC)

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

SHIRIKA la Nyumba la Taifa(NHC) limesema kwa kipindi kifupi wameweza kukusanya bilioni 5 kutoka katika wadaiwa ambao ni wapangaji wa nyumba za shirika hilo ambapo madeni yao yanafikia bilioni Bilioni 26.

Pia shirika hilo linakusudia kuyafuta madeni yanayofikia Bilioni 6  baada wadaiwa  kufa,pamoja na taasisi zilizopanga kwenye yumba ya shirika hilo kufirisika.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano NHC,Muungano Saguya ,wakati akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia kampeni ya kudai madeni ya kodi ya wadaiwa sugu waliopo na waliohama kwenye nyumba za shirika ilo,

Hata hivyo,Saguya amesema NHC limetoa miezi miwili kwa wapangaji wa nyumba za shirika hilo ambao wanamadeni wawe wamelipa ili kuepuka kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo kuchukuliwa mali husika za mdaiwa.

Hata hivyo,Saguya amesema katika oparesheni hiyo shirika ilo litashirikiana na vyombo vingine vya dola kuhakikisha linawasaka popote walipo wapangaji hao wanapatikana na kulipa kodi zao.

0/Post a Comment/Comments