NIMR YAWANUFAISHA WASHIRIKI 57 KUTOKA NCHI TANO KUHUSU TAFITI .

 



Na Issa Mohamed Dar es salaam

Email: issamohamed765@gmail.com

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuweka msukumo katika vipaumbele kwenye sekta ya Afya hasa kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu magonjwa ya binadamu ili kupunguza magonjwa.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mratibu wa maswala ya tafiti na machapisho, Idara ya afya ustawi wa jamii na lishe, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Dkt James Kengia wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku nne.

Dr. Kengia amesema katika mafunzo hayo wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja ikiwemo kufanya tafiti kwa maslahi mapana ya wananchi pamoja na kuzingatia maadili ya wakati wa kufanya tafiti.

‘’Tunao mfumo mzuri sana ambao ni wa uratibu katika ufanyaji wa tafiti katika sekta ya afya li kuhakikisha maadili yanazingatiwa kuanzia ngaz ya kitaifa yakiratibiwa na NIMR’’ Amesema Dr. Kengia

Kwa upande wake Mkurugenzi wa tafiti na machapisho kutoka chuo kikuu cha afya na sayansi shiriki, Bruno Sunguya amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu katika kuhamasisha maadili ya tafiti.

‘’Kwa ujumla washiriki hawa wanaenda kusaidia michakato  ya nchi zao ikiwemo kusimamia taratibu za maadili za kitafiti kwahiyo matarajio yetu watakua chachu katika kamati mbalimbali’’

Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya Taifa ya utafiti magonjwa ya Binadam nchini –NIMR, ambapo jumla ya washiriki 57 kutoka nchi ya Rwanda, Kenya, Uganda, Malawi na Tanzania wamepatiwa mafunzo lengo ni kuboresha kanuni na maadili ya tafiti za kitabibu pamoja na uwezo wa kudhibiti tafiti katika nchi hizo.

0/Post a Comment/Comments