POLISI WAONYA WALIOPANGA UHARIFU KILELE CHA MWENGE KAGERA

 






Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Na Daniel Limbe

JESHI la polisi nchini limewaonya wote waliojiandaa kufanya vurugu na uharifu mwingine siku ya kilele cha mwenge wa uhuru mkoani Kagera.

Kilele hicho kitaendana na sherehe maalumu ya kuzima mwenge wa uhuru kitaifa kwenye uwanja wa mpira wa Kaitaba mkoani humo,ambapo rais Samia Suluhu ndiye atakuwa mgeni rasmi katika tukio hilo.

Akitoa onyo hilo,Kamishina wa oparesheni na mafunzo kutoka makao makuu ya polisi,Awadh Haji, amesema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana  na watu wote waliojiandaa kufanya vurugu na uharifu mwingine na kwamba watakao bainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Askari polisi na askari wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama wapo katika maeneo mbalimbali ya mji wa bukoba na mkoa wa kagera kwa ujumla wanafanya doria ya miguu, magari, pikipiki, mbwa na boti ndani ya ziwa victoria...lengo ni kudhibiti vitendovyovyote vya uhalifu na wahalifu"amesema

Akizungumza na vyombo vya habari mkoani Kagera kuelekea kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Oktoba 14 mwaka 2022,huku akitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kushiriki kwa wingi pasipo kuwa na vizingiti vya kiusalama.

0/Post a Comment/Comments