Msemaji wa shirika la Posta Nchini, Elia Madules Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja akiwemo Meneja biashara ya barua na wasafirishaji -TPC Bwn. Jasson Kalile (Wakwanza kulia)

Baadhi ya menejimenti wa shirika la Posta Nchini wakifuatilia taarifa ya Msemaji wa -TPC, Elia Madules.
.....................
NA Issa Mohamed –Dare es salaam
Shirika la posta nchini –TPC limekusudia kutekeleza huduma zake ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na utalii.
Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam na Msemaji wa shirika hilo Elia Madules wakati akitoa taarifa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya posta Duniani yanayotarajiwa kuadhimishwa oktoba 09.
Amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan tayari –TPC linatarajia kuzindua stempu zitakazo sambazwa katika nchi takribani 192 inayoelezea sekta ya utalii.
‘’Matukio haya yote yatafanyika tarehe 09 oktoba 2022 ambayo ndiyo kilele cha maadhimisho kwahiyo kutakua na uzinduzi wa stempu ambayo inaongelea utalii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia’’ amesema Madules.
Kwa upande wake Meneja biashara ya barua na wasafirishaji –TPC, Jasson Kalile amesema kwa sasa shirika hilo limejikita katika kurahisisha mawasiliano ili kumuwezesha mwananchi kupunguza upotevu wa muda.
‘’Baada ya kugundua gape kubwa lililopo kwenye mawasiliano ya simu, mitandao ikiwemo ya kijamii na fedha shirika la posta limekuja na huduma ya duka mtandao ili kumsaidia mwananchi’’ Amebainisha Kalile
Umoja wa posta Duniani ulianzishwa Oktoba 9 mwaka 1874 huku Nchi ya Tanzania ilijiunga Machi 29 mwaka 1963 ambapo mpaka sasa umoja huo umetimiza miaka 148 tangu kuanzishwa kwake.

Post a Comment