WACHIMBAJI WADOGO MGODI WA MANDA MINING WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA GHARAMA ZA UTAFITI WA MADINI


Mmiliki wa mgodi mdogo wa Manda Asha Msangi
Mashimo yaliyopo ndani ya mgodi wa Manda

.........................

Na Richard Mrusha Kahama

WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Dhahabu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wamesema kuwa gharama za utafiti wa madini hayo ni kubwa jambo ambalo wachimbaji wengi wanashindwa kumudu hali inayosababisha uharibifu wa Mazingira.

Wamesema kuwa ipo haja ya Serikali kutafuta namna ya kusaidia wachimbaji hao kufanya utafiti wa upatikanaji wa madini hayo kuliko hivi sasa wanavyoendelea kufanya uchimbaji bila kufanya tafiti.

Akizungumza na waandishi wa habari leo OKtoba 21 mwaka huu waliofika kwenye eneo la Mgodo mdogo wa dhahabu wa MANDA MINING uliopo Mtaa wa MWIME kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama Asha Hassan Msangi mmiliki wa mgogi huo Amesema kuwa nivema serikali ikaliona hilo ili kulinda uharibifu wa Mazingira juu ya uchimbaji holela.

"Tunamuomba Waziri Mwenye dhamana kusimamia jambo hili kwani kuchimba sehemu ambayo haijapimwa inaleta uharibifu wa mazingira kwani kuchimba bila kufanya utafiti ni sawa na kufanya ramli ambayo mwisho wa siku inasababisha eneo husika kubaki mashimo "amesema Mama Asha Msangi

Ameongeza kuwa mchimbaji mkubwa anafanya tafiti za kina kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji jambo ambalo linamfanya kuwa na uhakika wa kile anachokitafuta kuliko wachimbaji wadogo ambao wanachimba kwa kubahatisha hivyo wanaiomba serikali kupitia Wizara ya Madini kuweza kuwawezesha vifaa vya kufanyia utafiti wa miamba yenye dhahabu.

Amefafanua kuwa Suala la ukosefu wa madini ya dhahabu linawaingiza kwenye hasara kubwa kwa kufukia mashimo pindi wanapochimba na kukosa madini hayo hivyo ili kuondoa changamoto hiyo nivema serikali ikaleta vifaa hata kwa kuwakopesha hatua ambayo itawasaidia kuyalinda mazingira.

kwaupande wake msimamizi wa Machimbo hayo Wilson Lukuwi amesema amezunguka katika migodi mingi lakini ni wanawake wachache ambao wamejiingiza kwenye tasnia ya uchimbaji hivyo anaiomba serikali inayongozwa na Rais Samia Hassan Suluhu kuweza kuwaangalia makundi ya wanawake kama Asha Msangi ambao wapo kwenye sekta ya madini kwani wanapambana na wengi wanaamini mwanamke hawezi kufanya shughuli za uchimbaji.

"Ombi langu kwa serikali ya awamu ya sita kuweza kuwasaidia wanawake kama hawa ambao wameingia kwenye madini kuweza kupata mikopo na kuhusu tafiti ili kuweza kuwekeza fedha nyingi lazima pawepo na taarifa sahihi ya upatikanaji wa madini hayo kwenye maeneo husika,hivyo wakina mama hawa wakipatiwa taarifa hizi za utafiti inakuwa ni fursa kwao kuwekeza zaidi na kuwasaidia wengi zaidi."amesema

0/Post a Comment/Comments