WAHITIMU UDSM WATAKIWA KUTAFUTA FURSA BADALA YA KUSUBIRI FURSA.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amejumuika kama Mgeni rasmi katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada ambayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada ambayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
Baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu katika katika Mahafali ya Hamsini na Mbili Duru ya Pili kwa Minajili ya kutunuku Digrii za Awali, Stashahada na Astashahada ambayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

........................

NA MUSSA KHALID

Wahitimu wa Shahada za awali,Stashahada na Astashahada katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam wametakiwa kwenda kutafuta fursa badala ya kusubiri fursa ziwafuate jambo ambalo sio rahisi katika ulimwengu wa Leo.

Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam katika Mahafali ya Hamsini na Mbili duru ya tatu ya chuo hicho ambapo Mkuu wa Chuo,Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku jumla ya wahitimu 2,091 digrii za awali,Stashahada na Astashahada huku wahitimu wa kike wakiwa asilimia 55 na wakiume ni Asilimia 45.

Akizungumza katika halfla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Willium Anangisye amewataka wahitimu hao kutambua kuwa elimu haiwezi kuwa chachu ya Mabadiliko yaliyokusudiwa kama haitatumika katika kutatua matatizo katika Jamii.

Aidha amewataka kutoshusha hadhi ya chuo Kikuu Cha Dar es salaam Kwa kufanya jambo lolote lisilofanana na sifa na umaarufu wake.

"Ni muhimu mkawa wepesi wa kujifunza Mambo mapya na kubadilika kwa haraka Ili musiachwe kuwa nyuma"amesema Profesa Anangisye 

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Balozi wa Mwanaidi Sinare Majaar amewasisitiza wanataaluma kufanya juhudi Katika kufanya tafiti Kwenye maeneo yatakayogusa maisha ya watanzania Ili ziweze kutoa majibu ya matatizo yaliyopo kwenye Jamii.

Amewataka kuwa waerevu katika kuzikabili changamoto za Maisha wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa za kuendeleza Maisha.

Nao baadhi ya wahitimu Katika Chuo hicho wamesema watakwenda kuhakikisha wanayafanyia kazi yote waliyojifunza sambamba na kutumia fursa ya kujiajiri na kuaniri wengine ili kujiongezea manufaa lakini kuunga juhudi za serikali katika kukuza uchumi wa nchi.

Hata hivyo wahitimu hao wamekumbushwa kutosahau kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma Katika kuutumikia umma wa watanzania.

Mahafali hayo yamehudhuriwa na wajumbe wa baraza la Chuo UDSM,Naibu Mkamu wa Chuo UDSM Prof Boniventure Rutinwa,Naibu Makamu wa Chuo UTAFITI Prof Benadeta Kilian na wengineo.

0/Post a Comment/Comments