WAKULIMA KANDA YA ZIWA WANUFAIKA NA MBOLEA ZA RUZUKU

Wakulima waliofurika ili kujipatia mbolea katika Halmashauri ya Wilaya Muleba iliyokuwa ikiuzwa na wakala wa kampuni la Yara Tanzania Limited leo tarehe 7 Oktoba, 2022. 
Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Kanda ya Ziwa Moro Ng'elenge akimshauri jambo mkulima mara baada ya kununua mbolea kwa bei ya ruzuku iliyokuwa ikiuzwa na kampuni ya uingizaji wa mbolea ya YARA Tanzania Limited leo tarehe 07 Oktoba 2022 
Wakulima waliofurika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Nyehunge Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ili kununua mbolea za ruzuku zilizokuwa zikiuzwa na wakala wa kampuni la Yara Tanzania Limited ambapo kiasi cha tani 4.5 kati ya zaidi ya tani 9 zilizofikishwa katika kata hiyo 

..................

Wakulima wa halmashauri ya Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza wameanza kunufaika na mbolea za ruzuku baada ya kampuni la Yara kuanza kuuza mbolea hizo kwa wakulima.

Aidha, wakulima wa Muleba wameanza kunufaika na mbolea hizo za ruzuku zinazouzwa na wakala ambapo wananchi walifurika ili kununua mbolea hizo.

Kiasi cha tani 9.3 za mbolea zilifikishwa katika halmashauri hiyo na kuuza tani 4.5 kwa wakulima wa Halmashauri ya Buchosa leo tarehe 7 Septemba, 2022 ukiwa ni mwelekeo mzuri kuelekea msimu wa kilimo 2022/2023
 

0/Post a Comment/Comments