WAMACHINGA DAR WALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KULIKABILI GENGE LA PANYA ROAD

Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph Namoto (katikati) wakati akitoa tamko la SHIUMA Kuhusu mikakati inayoendelea ya jeshi la polisi kulitokomeza genge la Panya Road.

..........................

NA SALYM BITCHUKA 

Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania SHIUMA limelipongeza na kulishukuru  jeshi la polisi na uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuchukua hatua za haraka na kuweka taratibu na mbinu mbalimbali za kukabiliana na genge la vijana wahalifu maarufu Panya Road  mkoani  hapa. 

Hayo yameelezwa leo  jijini  Dar  es  Salaam  na Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph Namoto wakati akitoa tamko la SHIUMA Kuhusu mikakati inayoendelea ya jeshi la polisi kulitokomeza genge la Panya Road. 

Aidha Namoto amekemea  baadhi ya wanajamii na baadhi ya wanasiasa ambao wanajaribu kubeza na kupotosha mchakato mzima  unaoendelea  wa  kupambana na  genge hilo la kihuni kitendo alichosema ni cha kupingwa kwa nguvu zote. 

Kwa upande wake Makamu  mwenyekiti wa Machinga Tanzania Steven Lusinde ametumia nafasi hiyo kuwaasa  vijana  kutokufanya  uhalifu  kwa  madai  kuwa hakuna ajira na badala yake kujiunga na Umoja wa Machinga kwani  ndani ya umoja huo kumekuwa na fursa za kutosha. 

Nao baadhi ya wenyeviti wa machinga  wilaya  akiwemo Mwenyekiti Machinga wilaya ya Ilala Bakari Saidi Makupa na Mwenyekiti machinga wilaya ya Kigamboni Faida  Nurdin Mohammed kwa pamoja wamepongeza kamati za ulinzi katika  maeneo husika huku wakiwataka wazazi na walezi  wa watoto ambao bado  wanaojihusisha  na vitendo hivyo   kutoa  taarifa  ama  kuwakemea  ili  waachane   matukio  hayo.

Hivi   karibuni  jeshi  la polisi  kanda  maalum  ya  Dar es  Salaam liliendesha  operesheni kamambe  iliyofanikiwa  kuwakamata  vijana  kadhaa  wa  genge  hilo  la panya  road  na baadhi  yao   kuuwawa.

 

0/Post a Comment/Comments