Viongozi wa Watetezi Uhai, Mkurugenzi wa Pro-Life Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kutetea Uhai Duniani, Human Life International kwa nchi za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza, Emil Hagamu; Mkurugenzi wa Pro-Life Uganda, Padri Jonathan Opio; Mratibu wa Vijana kutoka Jukwaa la Vijana Pro-life na Pro- Family kutoka Kenya, Tobioa Naruki; Mkurugenzi wa Pro-Life Rwanda, Aloys Ndengey; Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake kutoka Kenya, Dakta Wahome Ngare; na Mkurugenzi wa Taasisi ya ‘Citizengo’ Kanda ya Afrika, Ann Kioko kutoka Kenya wakiwa katika picha ya Pamoja nje ya Ofisi za Bunge mjini Kigali, Rwanda.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Frida Manga, Kigali.
Watetezi Uhai kutoka Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda wamekabidhi kwa Katibu wa Sipika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, John Mutega, majumuisho ya mazungumzo kati yao na Kamati ya Malengo ya Jumla ya Bunge hilo katika Ofisi za Bunge mjini Kigali nchini Rwanda.
Makabithiano hayo yamefanywa na Watetezi hao wa Uhai, baada ya kushindwa kuelewana na Kamati hiyo, ambapo Mwenyekiti wa Kamati, Dennis Namara, kwa kuzingatia kanuni za uendeshaji wa masuala ya malalamko alilazimika kurudisha suala hilo kwa Spika wa Bunge kwa uamuzi.
Watetezi hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Pro-Life Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai Duniani, (Human Life International) kwa nchi za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza, Emil Hagamu; Mkurugenzi wa Pro-Life Uganda, Padri Jonathan Opio; Mratibu wa Vijana kutoka Jukwaa la Vijana Pro-life na Pro- Family kutoka Kenya, Tobioa Naruki; Mkurugenzi wa Pro-Life Rwanda, Aloys Ndengey; na Mkurugenzi wa Taasisi ya ‘Citizengo’ Kanda ya Afrika, Ann Kioko kutoka Kenya.
Kwa mujibu wa utendai wa vikao vya Kibunge, ajenda ambazo hazitajadiliwa katika Bunge hadi ukomo wake, miswada yote ambayo haikujadiliwa itakuwa imetupwa kando; na kwa vile Bunge la 4 la Jumuiya ya Afrika Mashariki litafikia ukomo wake mnamo Desemba 2022, masuala yote yanayohusiana na Bunge hilo yatafikia ukomo. Mswada wa Ujinsia na Afya ya Kizazi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki nao utakuwa umefikia mwisho wake.
Watetezi hao wanayofuraha kwani juhudi zao za kupinga Muswada huo zimezaa matunda.
Taarifa za ndani zinaonyesha kuwa Muswada huo umesimamishwa si tu kutokana na Watetezi wa Uhai kuupinga bali pia baadhi ya Wabunge wa EALA kuupinga.
Aidha Watetezi hao walisema wamefarijika na Kauli za baadhi ya maofisa wa Bunge hilo kuwataka kutohangaika mswada huo ambao tayari umezikwa na badala yake washughulikie maswala mengine yanayogusa jamii.
Kwa mujibu wa Watetezi hao Muswada huo unavipengele ambavyo vinakwenda kinyume na Mila, Dini na Utu wa Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Miongoni mwa vipengele hivyo ni kile kinachotaka ama kinacholazimisha Nchi za Afrika Mashariki kufanya matumizi ya Vithibiti Mimba kuwa sehemu ya maisha ya watu bila kujali umri, wala hali ya Ndoa na hasa kulazimisha matumizi yake kwa watoto kwa kisingizio cha kuwawezesha watoto kumaliza masomo, bila kujali athari za matumizi hayo watoto.
Pia vipengele vinavyotaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga Sheria za Kutoa Mimba na kuingiza masomo ya elimu ya ngono (comprehensive sexuality education) ambayo imethibitika katika nchi nyingine kusababisha mmomonyoko wa maadili. Hali kadhali Muswada unazitaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutungua sheria za kuruhusu matumizi ya teknolojia saidizi ambapo uzao utapatikana bila kulazimika kuwa katika mahusiano ya mwanaume na mwanamke.


Post a Comment