WAZIRI AWESO AWATAKA WAKAZI DAR KUWA WATULIVU WAKATI WA MGAO WA MAJI


 .......................

NA SALYM BITCHUKA 

Waziri maji Juma Hamidu Aweso amewataka Wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kuwa watulivu wakati mamlaka ya maji safi na maji taka katika mkoa huo DAWASA ikiendelea kuweka utaratibu wa Mzuri wa wa upatikanaji maji ya mgao katika maeneo yao. 

Hayo ameyasema leo wakati wa ziara yake ya Kutembelea Ujenzi wa Uwekaji Valvu katika Bomba lilipo Maeneo ya Tegeta Nyuki mkoani Dar es Salaam ili liweze Kurahisisha Mgao wa Maji unaoratibiwa na DAWASA kutokana na upungufu wa maji.

Waziri Aweso amesema amefurahishwa na Kazi inayofanywa na Mafundi wanaofanya marekebisho hayo huku akiwataka DAWASA Kuhakikisha wanafanya mgao huo bila upendeleo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mafundi wanaendelea kukarabati valvu hilo usiku na mchana lengo ni kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kulingana na kiwango kilichopo.

Nae mkuu wa wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akizungumza katika ziara hiyo amesema mamlaka ya maji haitasita kushirikiana na wale wote wenye visima vya maji ili kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanapata maji ya uhakika katika wilaya hiyo.

Mkoa wa Dar es Salaam umepukuwa na upungufu wa maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi huku mamlaka husika ikiwataka wananchi kutumia maji kwa uangalifu huku ikiwasihi kuweka utaratibu mzuri katika ujenzi wa nyumba zao katika utunzaji wa maji.

0/Post a Comment/Comments