Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Richard Mrusha
Wasanii wa Muziki nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kongamano la Muziki la ACCES linaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 24 hadi 26 mwaka huu ili waweze kukutana na wanamuzii wa kimataifa na kubadilishana uzoefu.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo DKT Hassan Abbas wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema sekta ya sanaa na utamaduni inazidi kukua kwa kasi kutokana na Tanzania kuwa nchi ya 5 Afrika kufanyika kwa Tamasha hilo kubwa linalowahusisha wasanii wakubwa wakimataifa.
“NiTanzaniaTena; Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia jambo hili kubwa Afrika na linalowaleta wadau kutoka Afrika na kote duniani, imedhamini sehemu ya mkutano huu kwa nia ya kuwaletea karibu wasanii wetu fursa za kujua masoko makubwa zaidi na fursa za kujuana. na wakubwa zaidi, Sisi tumetimiza wajibu wetu,” Amesema Dkt. Abbasi.
na Kwa upande wake Mkurugenz wa Music in Africa Foundation Eddie Hatitye amesema lengo la mkutano huo na wanamziki ni kukuza vipaji na ubunifu wa wanamuziki, kutangaza na kukuza biashara kwa kukutana na wadau wa kimataifa wenye nia ya kufanya biashara ya mziki.


Post a Comment