AFRICAB YAAHIDI KUENDELEA KUZALISHA BIDHAA ZENYE VIWANGO BORA

 






Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


UONGOZI wa kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya Umeme cha Kilimanjaro Cables (AFRICAB) umeahidi kuendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora wa viwango vya juu  kwa lengo la kuwanufaisha wananchi sambamba na kuitangazaa nchi kimataifa.

Akizungumza Dar es Salaam, mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo Mohammed Ezzi, amesema  malengo ya kampuni hiyo kwa sasa ni kuhakikisha  bidhaa wanazozizalisha zinapambana na bidhaa za aina hiyo za kimataifa kwa lengo la kuzidisha ushindani. 

Kauli ya Mkurugenzi huyo imekuja siku chache mara baada ya Kampuni hiyo kushinda tuzo mbili ikiwemo ya mzalishaji bora wa vifaa vya nishati pamoja na mshindi wa jumla kwa kampuni zinazolisha vifaa vya umeme zilizotolewa na Shirikisho la Viwanda Tanzania(CTI) na kuzishirikisha kampuni mbalimbali nchini.

Akizungumzia hatua hiyo Ezzi amesema silku zote malengo ya AFRICAB ni kuzalisha bidhaa zinazozingatia matakwa ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na  kuendana na mahitaji ya wananchi hatua ambayo imeifanya kampuni hiyo kupendwa na wananchi hao sambamba na biidhaa inazozizalisha. 

“Tunawashukuru sana wananchi kwa kuendelea kutuamini, AFRICAB kampuni inayomilikiwa na sisi wazawa tutahakikisha hatuwaangushi kwa bidhaa zetu na zaidi tutazidi kushirikiana na Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzalisha bidhaa zenye ubora kwa lengo la kuongeza ushindani kimataifa” amesema Ezzi

Aidha amesisitiza kuwa uwepo wa Sera nzuri za uwekezaji chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kiasi kikubwa umeiwezesha kampuni hiyo kutimiza malengo yake ya uzalaishaji wa bidhaa hizo za umeme ambazo zimekuwa zikipata masoko katika mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki na kati.

Miongoni mwa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ni  pamoja na  Transfoma, nyaya za usambazaji umeme wa mkondo mkubwa, nyaya za umeme za majumbani, Taa mbalimbali, ‘Pipe’ switchi na vingine vingi ambavyo kimsingi vipo katika matumizi ya umeme.

ends

0/Post a Comment/Comments