Mkurugenzi wa usimamizi wa sekta ya fedha kutoka benki kuu nchini -BOT, Sadati Musa akizungumza Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa -KCB Cosmas Kimario akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa hatifungani ya "Fursa Sukuk
Mkuu wa idara ya benki ya kiislam -KCB, Amour Muro
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mitaji, masoko na dhamana -CMSA, Nicodemus Mkama.
...........................Na: Issa Mohamed –Dar es salaam.
Email: issamohamed765@gmail.com
Benki ya –KCB imekusudia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 10 kuanzia Novemba 9 hadi Disemba 5 mwaka huu kupitia hati fungani bila riba iliyopewa jina la fursa Sukuk lengo ni kuisaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa awali wa mauzo ya hatifungani, Mkurugenzi wa usimamizi wa sekta ya fedha kutoka benki kuu nchini –BOT, Sadati Musa amesema juhudi zilizofanywa na –KCB imeunga mkono dhamira ya serikali katika kupunguza umaskini kwa watanzania.
Pia ameziagiza taasisi za kifedha nchini kujikita katika kuleta huduma bunifu zitakazowasaidia wananchi ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo na kupunguza viwango vya riba ili kuleta uchechemuzi katika sekta ya fedha.
‘’Ni dhahiri kuwa juhudi hizi zinaendana na malengo ya serikali ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wananchi kupitia upatikanaji wa mikopo, serikali kupitia benki kuu Tanzania imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kupunguza viwango vya riba’’ Amesema Musa.
Naye mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mitaji, masoko dhamana –CMSA, Nicodemus Mkama amesema serikali imeweka mkakati katika sekta ya fedha ili kuja na ubunifu utakaoleta msukumo katika sekta hiyo.
‘’Serikali kupitia mpango wa maendeleo ya sekta ya fedha iliweka mikakati ya kuhakikisha inakuja na bidhaa ambazo zinakidhi matakwa ya wawekezaji, uzinduzi huu unaunga mkono mpango wa serikali wa miaka kumi’’ Amebainisha Mkama
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa –KCB, Cosmas Kimario amesema hatifungani hizo zitatumika kuendeleza idara ya –KCB Sahl inayotoa huduma za kiislam ikiwemo mikopo, huduma za miamala za benki na uwekezaji.
Hatifungani ya fursa Sukuk ni ya miaka mitatu ambapo Benki ya –KCB inatoa fursa kwa watanzania kununua hatifungani kuanzia shilingi laki tano na kuendelea huku kila mwaka asilimia 8.75 la gawio hutolewa
Mkurugenzi mtendaji wa -KCB Cosmas Kimario akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa hatifungani ya "Fursa Sukuk
Mkuu wa idara ya benki ya kiislam -KCB, Amour Muro
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mitaji, masoko na dhamana -CMSA, Nicodemus Mkama.Na: Issa Mohamed –Dar es salaam.

Post a Comment