CHAMA CHA ADC CHALIA NA HUJUMA ANAZOFANYIWA RAIS SAMIA SULUHU.


...................

SALIM BITCHUKA

Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimewataka watendaji na viongozi wote kushikana pamoja katika kumsaidi Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha matatizo ya Watanzania yanaondoka.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti  taifa wa chama cha ADC,Hamad Rashid wakati akifungua mkutano wa Bodi ya uongozi Taifa wa chama hicho.

Hamad Rashid amesema kumekuwa na baadhi ya watendaji wa serikali wakikwamisha baadhi utekelezaji wa miradi ikiwemo katika eneo la maji,umeme na bei ya Chakula kushindwa kujibu maoni  sahihi ya ufumbuzi  yanayowasilishwa kwao.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa ADC Doyo Hassan Doyo kupitia mkutano huo ametambulisha mabadiliko ya rangi za chama hicho  kutoka blue na kuwa rangi ya chungwa.

Chama cha Alliance Democratic  Change ADC kimekuwa ni miongoni mwa vyama vyenye usajili wa Kudumu kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa ambapo leo kulikuwa na mkutano Mkuu na wajumbe  wa bodi kikijadili ajenda Kumi na moja ambazo wanatarajibkuzitolea maamuzi.


 

0/Post a Comment/Comments