CHAMA CHA MAPINDUZI CCM SHAURI MOYO WAMPONGEZA SIDDE




......................

Na Heri Shaaban CCM Ilala )

Chama cha Mapinduzi CCM tawi la SHAURI MOYO Ilala kimempongeza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde na viongozi wa chama Kata ya Ilala waliochaguliwa akiwemo Mwenyekiti wa CCM Habib Nasser.

Akizungumza katika hafla hiyo katibu Tawi la CCM SHAURI MOYO Mwajuma Sultan alisema ushindi wa Mwenyekiti Said Sidde ni Faraja kubwa kwa Kata ya Ilala kwani Sidde amekifanyia mambo mazuri chama Cha Mapinduzi .

Katibu Mwajuma aliwataka Wanachama wa chama cha amapinduzi SHAURI MOYO kushirikiana na Viongozi wa chama hicho waliochaguliwa kwa ajili ya kujenga chama cha Mapinduzi CCM .

Alisema CCM Tawi la SHAURI MOYO wamejipanga vizuri kuakikisha CCM inashinda Viti vyote Serikali za Mtaa .

Akizungumzia hafla hiyo alisema kabla kuwapongeza viongozi wa chama kulikuwa na Matukio ya upimaji Afya ,uchangiaji wa Damu ,Ili kuokoa wezetu walio na uhitaji zoezi ambalo lilikuwa likisimamiwa na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Haji Bechina .

Akizungumzia uhai WA chama CCM SHAURI MOYO Lina wanachama 900 Wanachama wapya 200 ambao hawajapata kadi 350 waliosajiliwa kadi za kisasa kumekuwa na changamoto upatikanaji wa kadi za kisasa wa nachama wengi kadi  amna 

Akizungumzia Hali ya kisiasa wamekuwa wakishirikiana pamoja na Viongozi wa Jumuiya na chama ,mahusiano ya Serikali ya Mtaa na chama yapo vizuri wanashirikiana vema na Mwenyekiti wao wa Karume Haji Bechina ,Diwani Saady Khimji na Mwenyekiti wa CCM kata Habib Nasser .

" Dhumuni la sherehe hii ni kukupongeza kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala wewe ni mzaliwa wa Ilala tunakupongeza Mwenyezi Mungu akujalie hekima na upendo katika utekelezaji wa Majukumu yako na kujenga chama na Serikali "alisema Mwajuma .


Pia tunampongeza Diwani wetu Saady Kimji kuchaguliwa mkutano Mkuu CCM Taifa ,Mohamed Ally Balhabou kuchaguliwa ujumbe Kamati ya Utekelezaji Uvccm Wilaya.

Mwisho

 

0/Post a Comment/Comments