FURSA SEKTA YA GESI RUVUMA NA MTWARA TPDC KUSHIRKIANA NA KAMPUNI YA ARA.

 



Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Richard Mrusha

 Waziri wa Nishati,January Makamba, ameliasa  Shirika la Maendeleo la Petroli nchini(TPDC) na kampuni ya petroli ya ARA, kuhakikisha mradi wa uchimbaji wa gesi kitalu cha Ruvuma kilichopo mkoani Mtwara unamalizika kwa wakati.

Makamba ameyasema  hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa  halfa ya uwekaji saini mkataba wa yongeza wa  uzalishaji na Ugawanaji Mapato(PSA) kitalu cha Ruvuma-Mtwara.

 amesema dhamira ya serikali ni kuona mradi huo unakuwa na tija kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi na kupata fursa ya ajira ambayo italeta chachu ya maendeleo katika eneo hilo na kuweza kutoa ajira 10000 kwa watanzania

 Pia amesema anataka kuona unakamilika ndani ya miezi 12 na  hategemei kusikia mradi huo unachelewa kwa kile kinachotajwa kuwa  Fedha wakati fedha ya mradi ipo.

Makamba amesema mradi huo ukikamilika utakuwa mradi wa kwanza wa gesi kwa ukanda wa Afrika mashariki ambao utalinufaisha taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kupata kodi,tozo,Gawio kwa serikali,pamoja na serikali kupata kwenye maligafi.

Aidha,Makamba amesema pia wananchi wa mikoa ya kusini wanatarajia kunufaika wakati wa ujenzi wake ikiwemo kupata ajira wakati ujenzi wa mradi huo,.

Na kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa ARA petroleum Erhan Saygi ameishukuru serikali ya tanzania hususa ni viongozi wa serikali za vijiji kwa ushirikiano walioonyesha na kuongeza kuwa kukamilika kwa uwekezaji huo kutachagiza uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania hali itakayosaidia kukuza pato la wananchi na taifa kwa ujumla 

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio amesema kuwa uwekezaji huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 500 unatarajiwa kuzalisha takribani futi za ujazo milioni 160 kwa siku huku akiweka wazi kuwa utekelezaji wake utasaidia kuongeza chachu na kushashishi wawekezaji wengi zaidi

0/Post a Comment/Comments