
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini zinasaidia marubani kupata uelewa na kufahamu safari zao wanazokwenda ili kuepukana na madhara.
Kauli hiyo imetolewa na Rubani mstaafu ambaye amefanya kazi hiyo zaidi ya miaka 41, Edwin Magoti Mwijuma wakati akifanya mahojiano na Kituo hiki leo jijini Dar es salaam ambapo amesema marubani wamekuwa wakihangaika katika maeneo yenye hali ya hewa mbaya jambo linalofanya washindwe kumudu safari zao.
Edwin amesema hali ya hewa mbaya ambayo imekuwa ikiwasumbua marubani wamekuwa wakikutana nayo nje ya nchi ni pamoja na ukungu,mvua kunyeesha na Barafu ikiwa ni tofauti na kwa Afrika Mashariki.
‘Kwa Afrika Mashariki hali ya hewa mara nyingi inakuwa ni nzuri ila changamoto katika baadhi ya viwanja hakuna vifaa vya kuongoza mpaka chini kwa mfano siku moja nilikuwa natua nakaribia tu fisi wawili wanakatiza nikashindwa kutua hivyo inapotokea hivyo huwezi tua unaondoka’amesema Edwin
Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa wakiwa safarini Edwin amesema ni vyema rubani akawa na nidhamu ya kabla ya kwenda kurusha ndege kwa kutokuwa na matatizo,mawazo ili kuendana na safari.
‘Pia niwapongeze watu wa Hali ya Hewa kwani kwa hivi sasa taarifa tunazipata mpaka kwenye simu na wakati mwingine unaweza kupiga simu kuuliza hali ipo vipi katika maeneo flani ili kupata uhakika zaidi kabla kwenda kutuo huko’ameendelea kusem Edwin
Ikumbukwe Rubani huyo mstaafu mwaka 1999 ndiye aliyekwenda Ulaya kuuchukua Mwili wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage nyerere nchini Uingereza alipofariki wakati akipatiwa matibabu.

Post a Comment