TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA KIMATAIFA ICPD KUZINDULIWA ZANZIBAR .

Mwakilishi Mkazi UNFPA Tanzania Mark Bryan Schreiner

 ............,..............
NA SALYM BITCHUKA

Imeelezwa kuwa asilima 18 ya vifo vya Kinamama vinavyotokea Hospitali wakati wa Uzazi vinasababishwa na ujuzi hafifu kwa watoa huduma.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Shirika la Idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA yenye lengo la kujadili kuhusu mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo Duniani ICPD, ambapo kwa mwaka huu unatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar.

Akifungua warsha hiyo Mwakilishi Mkazi UNFPA Tanzania Mark Bryan Schreiner amesema ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ni lazima kuweza kutekeleza maazimio ya ICPD kwa kuwa ripiti bado zinaonyesha jangwa la sahara linendelea kuonyesha kuwa na changamoto kadhaa ikiwemo vifo vitokanavyo na uzazi, mimba za utotoni na wasichana kutoa mimba kwa njia isiyo salama.

Kwa upande wake mchambuzi wa masuala ya Idadi ya watu na Maendeleo kutoka UNFPA Tanzania Ramadhani Hangwa ametanabaisha kuwa wakati Dunia ikielekea kusheherekea mkutano wa ICPD 25 lakini bado kumeonekana uhitaji mkubwa wa utowaji wa elimu kuhusu Afya ya Uzazi kwa jinsia zote.

Aidha naye Mtaalamu Afya ya Uzazi ya mama na Mtoto kutoka UNFPA Felister Bwana amesema kupitia mkutano wa mwisho uliofanyika Nairobi nchini Kenya, Tanzania iliahidi kuongeza utolewa wa elimu kwa watoa huduma ya Uzazi Wakunga ambapo kwa sasa bado kunaoneka kuwepo kwa uhitaji wa huduma za dharura wakati mama anapojifungua.

Novemba 9 hadi 11, 2022 Tanzania kupitia Visiwa vy Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mkutano huo wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo ICPD ambapo Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio yaliyofikiwa Nairobi mwaka 2019 itapokelewa na Kuzinduliwa .

0/Post a Comment/Comments