JIJI LA DAR LAJIIMARISHA KATIKA UBORESHAJI WA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO.

 Mstahiki Meya na Mwenyekiti wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam hicho Omary Kumbilamoto akiongoza kikao hicho ambacho kimefanyika siku ya leo katika ukumbi wa AnatoglouKaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam Mhandisi Aman Mafuru akieleza dhamira ya kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es salaam

Diwani Mteule wa viti maalum katika Halmashauri hiyo Zainabu Bakari akila kiapo cha utii mbele ya wajumbe wa baraza la madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es salaam.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es salaam walioshiriki katika kikao hicho ambacho kimefanyika siku ya leo

...................

NA MUSSA KHALID

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaendelea na shughuli za ujenzi wa madarasa 310 ili kuhakikisha mwaka 2023 wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wanaingia katika madarasa hayo.

Hayo yamejiri leo katika kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ambacho kimeongozwa na Mstahiki Meya na Mwenyekiti wa kikao hicho Omary Kumbilamoto sambamba na Kuapishwa kwa Diwani Mteule wa viti maalum katika Halmashauri hiyo Zainabu Bakari.

Akizungumza na kituo hiki Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam Mhandisi Aman Mafuru amesema malengo yao ni kuhakikisha wananchi katika jiji hilo wanapata huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo sekta ya elimu.afya,na maendeleo ya jamii.

 ‘Sasa hivi tunaendelea na ujenzi wa madarasa kwani tuna jumla ya madarasa 310 na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametusaidia kiasis cha Tsh Bill 6.2 ambazo zinakwenda kujenga madarasa 310 ili mpaka kufuika mwaka 2023 wanafunzi waweze kuyatumia madarasa hayo.’amesema Mhandisi Mafuru

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo amesema mbali na hilo pia katika Halmashauri wanashughulikia hatua ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya Halmashauri ambapo inakwenda kulenga makundi ya vijana,wakina mama na watu wenye ulemavu ambapo wanapata uwiano wa asilimia nne,nne na mbili.

Katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wametumia fursa hiyo kueleza changamoto katika kata zao ambapo Diwani wa Kata ya Zingiziwa Maige Seleman Maganga wanakumbana na adha ya vivuko ambavyo havina ubora hivyo kuwa hatarishi kwa wananchi.

Diwani wa Kata ya Pugu Imelda Samjela akielezea adha wanayokumbana nayo kutoka katika Dampo la Pugu Kinyamwezi amesema endapo miundombinu ikafanyika vizuri kwa kukarabatiwa kisasa adha hiyo itapungua na hakutakuwa na moshi na harufu mbaya.

Hata hivyo kuhusu hoja ya Changamoto ya maji iliyoibuka katika kikao hicho,Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Mhandisi Mafuru amesema Dawasa wanaendelea kuhakikisha wanarekebisha ili wanachi wapate maji katika maeneo yao.

0/Post a Comment/Comments