KONGAMANO LA MUZIKI LALENGA KUTANUA WIGO WA SOKO LA KAZI ZA WASANII DUNIANI.

Miongoni mwa wasanii waliojitokeza katika semina ya awali kuelekea Kongamano la Muziki ( Access Music conference 2022) Siza Mazogele kushoto kwake Mwanamuziki mkongwe Komando Hamza Kalala pamoja na mdau wa Muziki John Kitime
Mdau wa Muziki Hassan  Msumari  akisikiliza kwa umakini semina fupi ya Muziki pamoja na ushawishi kupata wadhamini na masoko ya kimataifa kwa kazi za wasanii inayotolewa  na Mkufunzi wa Naamala Samson huku akiwasisitiza  wasanii kutumia kongamano hilo kama njia ya kupata fursa mbalimbali
Wasanii na wadau mbalimbali waliojitokeza katika semina ya  awali ya kuwanoa wasanii na kazi zao iliyofanyika jana Novemba 06 Jijini Dar es salaam

.........................  

Na.Khadija Seif,Michuzi TV 

WADAU mbalimbali wa Sekta ya Sanaa ya Muziki  wapigwa msasa kwa mafunzo ya awali kuhusu usimamizi wa masoko ya kazi za sanaa jana Novemba 06,2022 kuelekea  kongamano la Muziki(Access Music conference 2022) linalotarajiwa kufanyika kuanzia Novembe 24 hadi 26 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere  Jijini Dar es salaam huku ikihusisha wasanii wa Muziki Afrika Tanzania ikiwa nchi mwenyeji wa Kongamano hilo.

Aidha jukwaa hilo linatarajia kujenga uthubutu wa wasanii kujiamini katika kupambania masoko ya kazi zao ndani na nje ya nchi kutokana na mbinu za ushawishi watakazofundishwa kwa kipindi cha kongamano.

Nae Mkufunzi wa Semina hiyo Naamala Samson amewasisitiza wasanii kutumia kongamano hilo kama njia ya wao kutoka sehemu moja kwenda nyingine  wasiishie kuwa washiriki huku akiongeza kuwa serikali imeshafanya sehemu yake hivyo wasanii wachangamkie fursa hiyo katika kongamano hilo.                

"Huo ndio msingi wa kuendelea katika utekelezaji wa jambo lolote lazima uongozwe na wazo kuu kisha utafanikisha utekelezaji wake baada ya kupata ujuzi na mawazo ya kina kutoka kwa waliofanikiwa".  

 Hata hivyo baadhi ya mada zilizofundishwa na kukonga wasanii pamoja na wadau w sekta ya Muziki ni namna ya kujinadi katika masoko (branding) na mbinu za ushawishi kupata wadhamini,matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pamoja na kulinda taswira ya msanii. 

   Kongamano hilo ni la tano linatarajiwa kufanyika likiwa na lengo la kujenga uwezo wa wasanii ili waweze kufanikiwa kiuchumi kwa kuwakutanisha na wadau waliofanikiwa,kujenga uhusiano kisanii na wadau  wapya pamoja na kutanua wigo wa soko la kazi zao kidunia

0/Post a Comment/Comments