Imeelezwa
kuwa taarifa sahihi na Elimu sahihi kwa mama wajamzito zitasaidia kupunguza
vifo ya kinamama vitokanavyo na uzazi.
Hayo
yameelezwa leo na Dkt. Maiko Masasi kutoka kituo cha Afya Round Table Mbagala
jijini Dar es Salaam wakati walipotembelewa na uongozi wa Kampuni ya Hatua
Group Afrika inayosimamia program ya Busela yenye lengo la kuhamasisha uwepo wa
Afya bora kwa mama wajawazito hapa nchini.
Dkt.
Maiko Masasi amesema ameguswa na kazi inayofanywa na Busela kwa kutoa elimu ya
lishe, Mazoezi na elimu ya saikolojia, kitendo alichosema kitawezesha mama wengi wajawazito kujitambua wakiwa
kwenye hali hiyo.
Aidha
Daktari huyo kutoka kituo cha Afya Round Table Mbagala ametanabaisha kuwa
anaamini taarifa sahihi zitawezesha wakinamama wajawazito kupata huduma zilizo
sahihi,lishe iliyo bora huku akiweka wazi kuwa wimbi kubwa la kinamama
wajawazito wamekuwa na upungufu wa damu wakati wa kujifungua kitendo
kinachotokana na kukosekana kwa elimu ya kutosha ya lishe .
Kwa
upande wake Afisa Manunuzi ambaye pia ni
muelimishaji kutoka Busela Elly Julius
amesema endapo mama mjamzito ataandaliwa mapema kwa kufanya aina ya
mazoezi,lishe bora pamoja na kutayarishwa kisaikolojia kuna uwezekano
mkubwa wa mama mjamzito kujifungua salama .
Kampuni ya Hatua Group Afrika kupitia programu yake ya Busela imekuwa ikitoa elimu ya Afya ya uzazi na Mazoezi kwa mama wajawazito kwa kuwafuata katika vituo vyao vya Afya na nyumbani lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.


Post a Comment